Header Ads Widget

OJADACT YAIPOMGEZA SERIKALI KWA KUTHIBITI DAWA ZA KULEVYA

 



Na Neema Nkungu

Arusha


Chama cha Waandishi wa Habari wa Kuliga Vita Matukizi ya Dawa za kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kimeipongeza  Serikali kwa kuimarusha Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA) kwa kufanya kazi ya kupambana na dawa za kulevya kwa weledi.


Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa OJADACT Bwana Edwin Soko Jijini Arusha kwenye maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani.


Bwana Soko amesema kuwa, DCEA imekuwa ikifanya kazi kubwa kwenye mpambano ya dawa za kulevya na kufanikiwa kukamata watuhukiwa wengi wa dawa za kulevya.


Kwa sasa DCEA umekuwa ikifanya kazi kwa weledi sana pamoja  kuwaunganisha wadau wa mapambano ya dawa za kulevya pamoja , hii imesaidia kupunguza uingizwaji na usambazaji wa dawa za kulevya Nchini.


OJADACT pia imewashukuru wadau wake mbalimbali wanaofanya nao kazi wakiweno NSSF Mkoa wa Mwanza ambao wote wamekuwa mstari wa mbele kwenye kuisaidia OJADACT kufanikisha shughuli zake..


Maadhimsho hayo yalikuwa na kauli mbiu isemayo Zingatia utu boresha huduma za kinga na tiba.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI