Header Ads Widget

UWT KIGOMA WATAKIWA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

Agripina Buyogera Mwenyekiti wa UWT mkoa Kigoma akizungumza katika kikao cha kamati ya utekelezaji ya UWT wilaya Kigoma Mjini
Prisca Mapunda Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UWT mkoa Kigoma akiongea kwenye kikao cha wajumbe wa baraza la UWT wilaya Kigoma Mjini ikiwa ni sehemu ya ziara ya  kamati ya  utekelezaji ya Jumuia  mkoani Kigoma


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

JUMUIA ya wanawake ya CCM (UWT) mkoa Kigoma imetaka viongozi na wanachama wa Jumuia hiyo kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa iliyofanya ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi na maendeleo kwa Watanzania.

 

Mwenyekiti wa UWT mkoa Kigoma, Agripina Buyogera alitoa wito huo wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji ya Jumuia hiyo katika mkutano walioufanya Kigoma Mjini na kubainisha kuwa mkoa Kigoma nI mfano hai wa vitendo hivyo vya Rais Samia vya kutekeleza sera za kujenga uchumi na kuleta maendeleo.


Buyogera  alisema kuwa mkoa umefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya kiuchumi na maendeleo ambayo imeleta mabadiliko na maendeleo makubwa ya kiuchumi kwa mkoa na watu wake akieleza pia uanzishwaji wa vyuo mbalimbali vya elimu ambavyo vimeongeza chachu ya wananchi wa mkoa huo kuongeza viwango vyao vya elimu.


Akizungumza katika mkutano huo Mjumbe  wa Baraza kuu Taifa la Umoja wa wanawake wa CCM (UWT) Prisca Mapunda amewataka viongozi na wanachama wa Jumuia hiyo kujikita kwenye siasa za uchumi kwa kutumia Jumuia hiyo kuanzisha miradi mbalimbali itakayowawezesha kuingiza kipato.

 

Mapunda akiongea na wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Kigoma Mjini akiwa kwenye ziara ya kamati utekelezaji ya baraza hilo alisema  kuwa ni lazima viongozi na wanachama wa Jumuia hiyo wajitambue kwa kushiriki kwenye shughuli za uchumi na maendeleo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kigoma Mjini, Ahmed Mwillima alisema kuwa UWT ni jeshi kubwa ambalo halina budi kusimamia kwa vitendo utekelezaji ilani ua uchaguzi inayotekelezwa na serikali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI