JAMII imehimizwa kuchangamkia fursa za kibiashara zinazopatikana katika nishati safi ya kupikia hatua ambayo itaisaidia kupunguza athari za uharibifu wa mazingira zinazotokana na matumizi ya mkaa na Kuni.
Akizungumza katika kongamano la nishati safi ya kupikia lililoandaliwa na taasisi ya wanawake wafanyabishara Tanzania TABWA, Meneja masoko wa kampuni ya gesi ya Oryx, Peter Ndomba, alisema fursa ni kubwa katika biashara hiyo.
Alisema kwa sasa watumiaji wa nishati safi ya kupikia ni Asilimia tano na kwamba lengo la serikali ni kufikisha watumiaji zaidi ya Asilimia 80 kwa miaka kumi ijayo na kwamba jamii ikiwemo wajasiriamali fursa bado ni kubwa kuwekeza katika biashara hiyo.
"Mpaka sasa Watumiaji wa nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi ni Asilimia tano pekee na lengo la serikali ni kufikisha watumiaji zaidi ya asili 80 Kwa miaka kumi ijayo...hivyo fursa ni kubwa Sana ya kibiashara ni wakati Sasa wa jamii hususani vijana kuchangamkia"alisema
Aidha alisema ni vema wadau mbalimbali wa nishati safi kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na matumizi ya Kuni na mkaa ili kudhibitibi uharibifu wa mazingira unaochangia mabadiliko ya tabia nchi.
"Katika jitihada zetu za kuiunga mkono serikali ya kumtua mama Kuni kichwani, tumetoa gawa Bure mitungi zaidi ya 7,000 Kwa miaka miwili mfululizo na pia Leo tumegawa mitungi 200 Kwa wajasiriamali walishiriki kongamano hilo wadau wengine waendelee kuisaidia serikali"alisema
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Wafanyabishara Wanawake Tanzania TABWA Noreen Mawala, aliitaka jamii kubadilika na kuanza kutumia nishati safi Kwa ajili ya matumizi ya kupikia ili kukabilana na athari za ubaribifi wa mazingira.
0 Comments