Header Ads Widget

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA VYUO VILIVYOPO MKOANI KIGOMA KUPELEKA VIJANA WAO ILI WAWEZE KUPATA TAALUMA MBALIMBALI

 


Mkurugenzi mkuu wa Chuo cha utangazaji UBA Baruan Muhuza na Mgeni Rasmi Katibu tawala Deogratius Sanga wakiwa wameketi moja ya studio za kisasa zilizopo chuoni hapo


NA Editha Karo,Matukio Daima App Kigoma

WAZAZI na walezi wametakiwa kutumia fursa iliyopo sasa katika Mkoa wa Kigoma kwa kutumia vyuo vilivyopo Mkoani humo kuwapeleka vijana wao kupata elimu na taaluma mbalimbali zinazotolewa na vyuo hivyo.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa chuo cha utangazaji cha ujiji Broadcasting Academy(UBA) Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye  alisema kuwa wazazi na walezi wanatakiwa kutumia fursa kama hizi adimu zinazopatika  Mkoani ya kuwapeleka vijana wao kupata elimu na taaluma mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo hii itasaidia vijana kupata maarifa na ujuzi.


Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Deogratius Sanga Katibu tawala msaidizi aliupongeza uongozi wa chuo cha UBA pamoja na bodi yake kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa chuoni hapo na kuleta chuo hicho mkoani hapa kwa wakati sahihi.

Mkurugenzi mtendaji mkuu wa chuo cha utangazaji UBA Baruan Muhuza akimuonyesha mgeni rasmi katibu tawala Msaidizi Deogratius Sanga moja ya darasa la kompyuta la kisasa chuo hapo


“Nampongeza Mkurugenzi mkuu wa chuo hiki ndugu Baruan Muhuza kwa uwekezaji huu mkubwa alioufanya,hiki ni chuo cha kwanza cha utangazaji katika Mkoa wetu na ni chuo cha kisasa naamini wanafunzi watakaosoma hapa watakuwa waandishi mahiri katika sekta ya uandishi wa habari” Alisema



Andengenye alisema serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu imeweka mazingira bora kwa wawekezaji katika nyanja zote hivyo serikali inaendea kuwakaribisha wawekezaji zaidi kuja kuwekeza kigoma katika nyanja mbalimbali.


“Nimefurahishwa na uwekezaji huu mkubwa wa elimu ndani ya Mkoa wetu ufunguzi wa chuo hiki utafungua fursa mpya ndani ya Mkoa wetu,muda wowote mkihitaji jambo lolote toka serikalini,ushauri karibuni milango ya ofisi yangu ipo wazi”alisema


Naye Kaimu Ofisa Elimu wa Mkoa Samson Shija alisema kuwa sekta habari na mawasilino nu sekta muhimu kwani imekuwa kama daraja la kuunganisha wananchi na serikali,aliwaomba wadau kukitumia chuo hicho ili kupata vijana walisoma taaluma ya utangazaji kwa weledi.


Kwa upande wake katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma(CCM)Mobutu Malimaalimpongeza Mkurugenzi mkuu wa chuo hicho Baruan Muhuza kwa kuwekeza katika taaluma ya habari ili kuweza kupata vijana wenye weledi na taaluma katika kazi hiyo.


“Hili ulillolifanya Mkurugenzi Mkuu wa chuo cha UBA ndugu Baruan Muhuza lipo kwenye ilani yetu ya chama cha mapinduzi upande wa elimu,naamini chuo hiki kitakuwa kizuri na bora kwa ukanda wetu wa Magharibi”alisema


Mkurugenzi mtendaji wa UBA Baruan Muhuza ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha azam TV alisema kuwa yeye ndo mmiliki mkuu wa chuo hicho kwa asilimia zote mia moja.


“Nilikuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuwekeza katika chuo cha utangazaji hatimaye namshukuru Mungu ndoto yangu imekuwa kweli,na mradi huu kila kitu nina miliki mimi kwa asilimia mia moja”alisema Mkurugenzi mkuu wa UBA


Alisema zaidi ya shilingili milioni 204 zimetumika katika uwekezaji hapo chuo ikiwa ni pamoja na kununua vifaa vipya vya kisasa kwa msukumo wap ni elimu kwa vitendo.



“Nina watu wote toka ndani ya Mkoa wa Kigoma na nje ya mkoa hata nchi za jirani  waje kwani chuo kina ithibati ya serikali,hivyo chuo hiki ni chenu tukitumie tupate watangazaji mahari kama mimi na waandishi mahari”alisema Baruan

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI