WADAU wa michezo manispaa ya kinondoni kata ya Mbweni wametoa wito kwa shirikisho la mpira nchini Tanzania (TFF) kuwekeza katika ligi za vijana ili kutengeneza soko la ajira kupitia mpira wa miguu
"Tunatoa wito kwa TFF na vyama vya michezo vya Wilaya kutilia mkazo ili kuibua wanamichezo mahili nchini, na kuongeza soko la ajira"
Mwenyekiti wa CCM kata ya Mbweni Abdulkadir Mgheni amesema ligi hii ni mwanzo mzuri ya kuwajali vijana na Chama Cha Mapinduzi kipo tayari kuanzisha ligi kama hii kila mwaka na kubaini vipaji kwa vijana, ameongeza kuwa mechi zote zitachezwa katika uwanja Mbuyuni mtaa wa Mpiji katika ligi inayoendelea ya CCM MBWENI SUPER CUP kwa kushirikisha timu za kata ya Mbweni ambazo ni Mbweni fc, Mpiji Fc, Maputo fc, Malindi fc, Teta fc na Geza fc
0 Comments