Header Ads Widget

WAZAZI CHANZO CHA TABIA MBAYA ZA WATOTO

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma


IMEELEZWA kuwa wazazi kushindwa kuwajibika katika matunzo na malezi ya watoto wao imekuwa na mchango mkubwa kwa watoto hao kujitafutia mahitaji yao na kusababisha kujiingiza kwenye vitendo vya uvunifu wa maadili na uhalifu.


Mkuu wa Mkoa Kigoma,Thobias Andengenye alisema hayo wakati wamaadhimisho ya kimkoa ya siku ya Kimataifa ya Familia iliyofanyika manispaa ya Kigoma Ujiji na kusema kuwa wazazi hali duni ya familia imekuwa ikichukuliwa na wazazi wengi kuacha kutekeleza matunzo na malezi ya watoto wao.


Kutokana na hilo alisema kuwa jamii inao wajibu mkubwa wa kutafakari hatua za kuchukua katika kukabiliana na hali hiyo ikiwemo mmomonyoko wa maadili kwenye jamii na kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

 


Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Kigoma, Salum Kalli  alisema kuwa pamoja na mikakati mbalimbali ambayo inatekelezwa mkoani humio kupitia Mpango wa Taifa wa kupinga Ukatili (MTAKUWA) bado vitendo vya ukatili vinaendelea mkoani humo ambapo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita matukio 3260 yaliripotiwa.




Akitoa neno la Tafakari katika maadhimisho hayo Katibu wa CCM mkoa Kigoma, Mobutu Malima alisema kuwa wazazi wanapaswa kujitafakari kwa hali zote zinazotokea kwenye jamii kwa tabia, mila, mienendo na matendo yapo kwenye nafasi ipi katika kuwalea watoto.

 

Malima alisema kuwa matendo mabaya yanayofanywa na watu wengi chimbuko lake ni malezi ambayo watu hao walipata kutoka kwa wazazi wao hukui wengi wakiachwa kutolelewa kwenye misingi ya kumjua Mungu.

 


Naye Paroko wa parokia ya jimbo kuu la Kigoma la Kanisa Katoliki, Castus Rwegoshora alisema kuwa athari za mafanikio mazuri ya familia yanaanzia kwenye matunzo ya watoto kwenda shule na kufuata mienendo ya dini ambayo huzaa upendo na kujali wengine.

 

Padre Rwegoshora alisema kuwa kama familia inalea watoto kwenye malezi yenye ukatili, ugomvi, ulevi wa kupindukia ni wazi malezi ya watoto yatafuata mienendo hiyo na siyo ajabu kukutwa wanapokuwa wakubwa wanakuwa na mambo ya ajabu ajabu ambayo hayazingatii maadili.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI