Header Ads Widget

WAFANYAKAZI WANAPASWA KUTAMBUA UMUHIMU WA

 



Na Mwandishi wetu. WHMTH


Kaimu Mkurugenzi na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Suleiman Mvunye amesema kuwa wafanyakazi wanapaswa kutambua umuhimu wa siku hii kwani inawapa nafasi ya kuwasilisha maoni yao kwa serikali kupitia vyama vyao.


Amezungumzia mfumo wa Anuani za Makazi kuwa ni mradi ambao umesaidia kuunganisha nchi nzima na kurahisisha upokeaji na utoaji wa huduma pamoja na masuala ya ulinzi na usalama.


“Leo hii ikitokea nyumba imeungua eneo lolote inakuwa rahisi kufikiwa kwa sababu mfumo wa anuani za makazi umerahisisha ufikiaji wa maeneo mbalimbali,"amesema Mvunye



Ameyazungumza hayo leo Mei 1,2023 Jijini Dodoma ,wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.



Naibu Waziri ,Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Mhe.Jumanne Sagini ametoa wito kwa Wafanyakazi wote, mbali na kazi zao za msingi za kila siku wanazozifanya kutosahau kuungana kwa pamoja katika malezi ya watoto na kusimamia maadili mazuri ili kutengeneza kizazi kizuri kwa ujenzi wa taifa.


"Najua tuna kazi nyingi ila tusisahau jukumu letu la msingi la malezi hili haliepukiki na tukizembea haya tutatengeneza kizazi ambacho hakitakuja kusaidia jamii wala taifa kwa miaka ijayo,"Amesema Mhe.Sagini



Pia Sagini amewataka waajiri kuhakikisha wanawasilisha michango ya waajiriwa wao kwenye mifuko ya uhifadhi wa jamii kwani kutokufanya hivyo wanawanyima haki ya msingi waajiriwa wao na kusababisha misuguuano yanapotokea matatizo.


"Na nyie Mifuko ya jamii msikae kimya kwa waajiri ambao hawapeleki michango na msisubiri mpaka mtumishi afariki ndio muanze kufuatilia kwa sababu sio sawa shughulikieni haya mapema ili kuepuka na minong'ono,"amesisitiza Mhe.Sagini



Aidha amewataka waajiri kuacha tabia ya kuwachagulia wafanyakazi vyama vya wafanyakazi vya kujiunga navyo kwani kufanya hivyo ni kuwanyima uhuru wao kwani kila mfanyakazi ana uhuru wa kuchagua ni Chama gani ajiunge nacho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI