UMOJA wa Jumuia ya wazazi CCM Taifa umepongeza jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan kwa kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii nchini.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (MNEC) kupitia jumuia ya wazazi CCM anaeyewakilisha viti wili Zanzibar, Habiba Ally Mohammed, aliyasema hayo, alipokuwa akizungumza na Zanzibar Leo, baada ya kumaliza ziara ya Jumuiya hiyo ya kutembelea hifadhi ya Taifa Tarangire iliyopo Mkoani Manyara.
Alisema kutokana na jitihada za Rais Samia ambazo amezifanya Katika sekta ya utalii ikiwemo filamu ya Royal Tour zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuhamasisha sekta hiyo Katika hifadhi mbalimbali za Taifa kwani kumekuwepo na ongezeko kubwa la watalii kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Alisema kumekuwepo na ushirikiano mkubwa kati ya Rais wa Tanzania Samia suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kuhakikisha wanahamasisha kuwepo kwa watalii wengi nchini hali ambayo inachangia ukuaji wa pato la Taifa kupitia sekta ya utalii.
Hivyo, aliwataka wananchi wa Tanzania kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi mbalimbali za Taifa ili kusaidia ukuaji wa sekta ya pamoja na kujionea rasilimali zilizopo Katka hifadhi hizo.
Pamoja na hayo, MNEC Habiba, alihisishi jamii ya kitanzania kuepukana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili ikiwemo kupinga vikali na jutojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ikiwa ni pamoja na kutoiga tamaduni za mataifa ya nje na badala yake kuendana na maadili ya kitanzania.
Aidha alisema katika kuabimisha wiki ya wazazi kitaifa ambayo inafanyika katika mkoa wa manyara, wilaya ya babati, alikagua miradi mbalimbali na utekelezaji wa ilani ya CCM kwenye maadhimisho hayo.
Alisema kuwa ilani ya CCM imekuwa ikiendelea ambapo hali ya maendeleo yamefikiwa kwa wannachi waliowengi jambo ambalo ni la kuendelewa kupongezwa kwa viongozi wa nchi ambapo ilani wamekuwa wakiitekeleza kwa vitendo.
Sambamba na hayo, Habiba alisema kuwa amepanda mti wa kumbukumbu kwenye viwanja vya skuli ya msingi Singe kama ishara ya kutunza mazingira na kuwasisitiza wananchi kuendelea kutunza mazingira ili kuepuka na uharibifu wa tabianchi ambalo ni janga.
0 Comments