Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Waandishi habari mkoani Njombe wametakiwa kutumia Kalamu zao na nafasi walizonazo kuandika habari zinazoufahamisha ulimwengu juu miradi mbalimbali inayopatikana mkoani hapa.
Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Njombe Erasto Mpete akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari katika mkoa wa Njombe.
Baadhi ya wadau wa habari waliohudhuria Maadhimisho hayo akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Njombe Ally Mhagama na Wilfred Willa mkuu wa Dawati la jinsia mkoa Njombe wamesema waaandishi wa habari wajikite kuandika habari zenye ukweli.
Mwakilishi wa wamiliki wa vyombo vya habari mkoani Njombe ambaye ni Mkurugenzi wa Uplands fm Humphrey Milingi amekumbusha wanahabari kufanya kazi kwa bidii ili wapate masilahi mazuri.
Mwenyekiti wa chama cha waaandishi wa habari mkoa wa Njombe Damiani Kunambi amewasihi wanahabari kufanya kazi kwa upendo huku akiwapongeza wadau kwa kupaza sauti juu ya masilahi ya waandishi habari.
Nao baadhi ya waaandishi wa habari mkoani Njombe akiwemo Tatu Abdala,Emmanuel Kalemba na Diksoni Kanyika wamewaomba wadau wawe wanatoa ushirikiano kwa wanahabari ili wafanye kazi bila ya vikwazo.
Siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani huadhimishwa May 3 kila mwaka, Kwa mkoa wa Njombe maadhimisho hayo yamefanyika leo yakiambatana na kauli mbiu isemayo"Kuunda mustakabali wa haki,Uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha haki nyingine za kibinadamu"
0 Comments