Na Amon Mtega
Songea.
BAADHI ya Wakazi wa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wameendelea kuyafurahia bidhaa mbalimbali ikiwemo maziwa yanayotengenezwa na kampuni ya Asas iliopo Mkoani Iringa.
Akizungumza Mederus Kavishe mkazi wa Manispaa ya Songea ambaye ni mmoja ya wauzaji wa bidhaa za maziwa ya kampuni ya Asas pamoja na Yoghurt amesema kuwa bidhaa hizo zimekuwa zikipendwa na baadhi ya wakazi wa Manispaa hiyo.
Kavishe akizungumzia kwa upande wa maziwa na Yoghurt amesema kuwa bidhaa hizo zimekuwa zikipendwa na watu wa lika zote na kuifanya bidhaa hiyo kutumika karibu kila familia.
Amesema kuwa bidhaa hizo zinaonyesha zinatengenezwa kwa ubora na kwa kuviwekea vionjo mbalimbali jambo ambalo hufanya kila anayetumia kuvutiwa na bidhaa hizo.
Mwisho.
0 Comments