Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Watanzania wametakiwa kukumbuka asili ya maeneo wanakotoka pamoja na kuenzi lugha za asili kwani itasaidia kutunza mila na tamaduni za kiafrika.
Katika uzinduzi wa kitabu cha lugha ya Kipangwa kinachoitwa ''Inyumba Mahame,Tuvuye Kunyumba''kilichoandikwa na mwandishi Gastor Mtweve mkazi wa Ludewa imeelezwa kuwa watanzania wengi wamekuwa walowezi katika maeneo wanayokwenda kutafuta maisha na kusahau kwao jambo ambalo linaondoa thamani ya tamaduni za kiafrika.
Akizindua kitabu hicho kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe,Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema ipo haja ya kitabu hicho kupelekwa katika shule za msingi ili watoto wajifunze asili zao huku akitaka kila mmoja kuenzi cha kwao.
Michael Mshindo ni mzee wa mila za Kipangwa ambaye anakiri kumfahamu vizuri mwandishi wa kitabu hiki huku akimtaja kama kijana aliyekuwa na akili nyingi.
Washiriki wa uzinduzi wa kitabu hicho akiwemo Bryn Shoo,Bertha Nyigu na Gwamaka Mwamasage ambaye ni mwandishi wa vitabu vya Liwaya mkoani Njombe wamesema kitabu hicho kimeikumbusha jamii ya kitanzania Kukumbuka waliko toka.
0 Comments