Header Ads Widget

RAIS SAMIA HALALI USINGIZI KWA AJILI YA WATANZANIA

 


NA RAYMOND MINJA IRINGA

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema matamanio ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona kwamba Changamoto mbalimbali za wananchi kwenye maeneo yao zinatatuliwa na kuleta matokeo chanya kama ilivyokusudiwa. 


Komredi Chongolo ametoa kauli hiyo wilayani mufindi wakati akiendelea na Ziara yake ya Siku 7 mkoani Iringa  ili kukagua uhai wa CCM pamoja na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm ya 2020/2023. 


"Mwenyekiti wa CCM ambae ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halali usingizi kutokana na changamoto nyingi zinazohitaji kutatuliwa ili nchi iweze kupiga hatua katika maendeleo" amesema Chongolo. 


Amesema kwa Sababu ya Dhamira njema kwa Watanzania ambayo inaoneshwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha matokeo chanya yanaonekana, Chongolo amewataka viongozi wilayani Mufindi kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza wananchi na kutatua changamoto zinazowakabili.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI