Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso Amesema katika eneo ambalo Wizara ya maji haijafanya vizuri nipamoja na eneo zima la usafi wa Mazingira kwani hata uwekezaji wake haujawekwa vizuri wa uondoshaji maji taka katika Jiji la Dodoma.
Akizungumza leo jijini Dodoma mara baada ya kushuhudia Utiaji saini Kati ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) mkataba wa Usanifu na Usimamizi wa Ujenzi wa Mradi wa kuboresha huduma ya Uondoshaji na kutibu MAJITAKA na Kampuni ya DOHWA Kutoka Nchini Korea ya Kusaini Waziri huyo amesema majitaka yasipowekewa utaratibu mzuri inaingia katika eneo zima la uchafuzi wa Mazingira.
Waziri Aweso amesema asilimia 20 ya wakazi wa Dodoma wanapata huduma ya uondoshaji majitaka ambapo katika ya wakazi hao kata 14 kati ya 41 ndio wanapata huduma ya majitaka kupitia mtandao wa DUWASA uliopo, ambao ufanisi wake hauendani na ongezeko la kasi la watu katika Jiji la Dodoma na uzalishaji wa Majitaka.
"Asilimia 80 ya Majisafi yanayotumika na binadamu katika matumizi yake ya kila siku hugeuka kuwa Majitaka sasa tujiulize yanakwenda wapi zaidi ya kwenda kuchafua Mazingira?,"amesema Aweso
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph amesema kuwa gharama za mradi huo kwenye Usanifu na Ujenzi unategemea kugharimu kiasi cha Dola za Marekani Milioni 70 sawa na Shilingi Bilioni 164.85 za Kitanzania.
Mhandisi Aron amesema ,Mkataba wa Usanifu na Usimamizi wa Ujenzi wa Mradi huo utagharimu kiasi cha Dola za Marekani 5,225,000 sawa na takribani Shilingi Bilioni 12.3
"Mradi huu unalenga kuhusisha Usanifu na ujenzi wa Mabwawa mapya makubwa 16 yenye uwezo wa kutibu takribani lita milioni 20 kwa siku,usanifu na ujenzi wa bomba kubwa (trunk main) kwa kilometer 107.5,ubadilishaji wa bomba chakavu kilomita 2.6 na ukarabati wa Kilomota 2.1 za Mtandao wa majitaka,"amesema Mhandisi Aron
Aidha Amesema ,Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha Miezi 49 ambapo awamu ya kwanza Mhandisi Mshauri atafanya kwa muda wa miezi 13 kusanifu Mradi na awamu ya atatumia miezi 36 katika ujenzi wa Mradi huo.
0 Comments