Header Ads Widget

RC MAKALLA: RAIS DKT, SAMIA SULUHU HASSAN NI KIELELEZO SAHIHI CHA MUUNGANO

 



- Asema Muungano wa Tanzania ni wa mfano duniani, haujawahi kuterereka Na chini ya Rais Dkt, Samia utaendelea kuimarika.


- Aeleza mafanikio lukuki ya muungano ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo.


- Asema Rais Samia amekusidia mwendokasi ifike mpaka Vikindu, fedha Bilioni 9 kujenga Hospitali Mbagala kuu.


- Awataka Wananchi kuenzi Na kulinda muungano.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla leo ameongoza Wananchi wa Mkoa wa huo kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo ametoa wito kwa Wananchi kusimama na Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kuuenzi na kudumusha Muungano.


Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika Uwanja wa Zakhem Mbagala, RC Makalla amempongeza Rais Dkt, Samia kwa kuwa kielelezo kuzuri Cha Muungano ambapo amesema ndani ya Miaka 59 yapo Maendeleo na Mafanikio Makubwa yaliyofanyika.


Aidha RC Makalla ametumia maadhimisho hayo kumuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Temeke na Meya wa manispaa hiyo kuhakikisha ujenzi wa Stendi ya kisasa ya mabasi ya Kusini* unafanyika ambapo pia amesema *Rais Dkt, Samia ametoa kiasi Cha Shilingi bilioni 9 kwaajili ya ujenzi wa Kituo Cha Afya Mbagala Kuu.



Kuhusu suala la kero za Muungano, RC Makalla amempongeza Rais Dkt, Samia kwa kuendelea kuzishughulikia mpaka Sasa zimebaki kero nne pekee.


Hata hivyo RC Makalla amesema maadhimisho hayo kiomkoa yanaenda sambamba na Uzinduzi na uwekezaji wa mawe ya msingi kwenye Miradi mbalimbali ya Maendeleo yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi bilioni 23  mpaka April 29.



Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano yameenda sambamba na kauli mbiu isemayo "Umoja na Mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu."

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI