Header Ads Widget

ANDENGENYE ATOA NENO MIAKA 59 YA MUUNGANO

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amewataka wananchi wa mkoa Kigoma kulinda amani, Umoja  na mshikamano uliopo ambao umekua nguzo kubwa ya kuhakikisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umedumu hadi sasa.

 

Mkuu huyo wa mkoa alisema hayo akizungumza na viongozi na wananchi wa wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma katika maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano ambapo kimkoa umefanyika wilayani Buhigwe.




Andengenye alisema kuwa siyo kazi rahisi kuwa na muungano kama huu ambao umedumu kwa miaka yote hii lakini hili linatokana na waasisi wa muungano huo Hayati Mwalim Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume walivyowajenga Watanzania kuwa wamoja wenye kupendana, kushirikiana na kutatua changamoto zao kwa njia za mazungumzo badala ya vita.

 


Kabla ya kuzungumza kwenye mkutano na viongozi na wananchi wa wilaya Buhigwe pia maadhimisho yaliyohudhuriwa na viongozi waandamizi wa serikali na taasisi zake kutoka wilaya zote za mkoa huo, Mkuu huyo wa mkoa ametaka kutunzwa kwa  miradi mbalimbali inayoanzishwa mkoani humo ili iweze kuwahudumia wananchi kwa muda mrefu.

 



Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa mradi huo ni sehemu ndogo ya miradi mingi inayotumia mabilioni ya shilingi kutekelezwa chini ya serikali ya awamu ya sita ya Raisi Samia Suluhu Hassan lengo likiwa kuondoa kero na kuleta maendeleo kwa wananchi hivyo haiingii akilini kuona wananchi wanaoletewa miradi ndiyo wanaoihujumu na kufanya isiweze kufanya kazi.

 

Alisema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ni matokeo ya amani, umoja na mshikano uliopo nchini unaochagizwa na kuwepo kwa amani na usalama hivyo akatoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanalinda amani na usalama uliopo ili nchi iweze kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

 



Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wa maji Meneja wa Wakala wa Maji Mijini na Vijijini (RUWASA) wilaya ya Buhigwe, Mhandisi Golden Katoto alisema kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 kinatarajia kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

 

Mhandisi Katoto alisema kuwa mradi huo utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 1.9 kwa siku utawezesha kunufaisha wananchi 14,378 wa vijiji vinne vya Buhigwe, Kavomo, Murela na Bwega na kwamba mradi ulipaswa kukamilika Februari mwaka huu lakini mkandarasi ameongezewa muda hadi mwezi Juni mwaka huu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI