Na HADIJA OMARY LINDI
Mbunge wa kuteuliwa mkoani Lindi Riziki Lulida ameungana na watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo walemavu wazee na mayatima katika kupata futari ya pamoja.
Tukio hilo limefanyika jana kwenye viwanja vya Ilulu ambapo pamoja na makundi hayo maalumu pia waumini wengine wa dini ya kiislamu waliweza kupata futari hiyo .
Akizungumza baada ya ifari hiyo shekhe Mkuu wa Mkoa huo Mohamedi Mushangani aliwasihi waislamu kuendelea kufanya ibada ya funga kwani ni moja kati ya nguzo tano za uislamu kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha quran tukufu.
Alisema muislamu yeyote ambae amejaaliwa uzima na kwamba hana tatizo lolote la kiafya anapaswa kuitekeleza nguzo hiyo muhimu ya uislamu Kwani saumu ni mkombozi kwa waislamu hivyo ikifika mwezi wa ramadhani inapaswa wafunge kweli kweli ikiwa pamoja na kufanya mambo mema na mazuri.
“zipo hadithi zilizotelemshwa kwa mitume na maswahaba wetu zikieleza yeyote atakaefunga ramadhani hali ya kuamini kulipwa heri na kutaraji kupata thawabu basi huyo mungu atamsamehe makosa yake yote aliyoyatanguliza lakini mwenye kula mchana wa siku moja tu ya ramadhani pasipo na sababu yoyote iliyomfanya ale mchana mtu huyo hawezi kulipa saumu yoyote ya kuilipisha siku ile aliyofungua pasipo sababu hata kama atafunga mwaka mzima” Shekhe Mushangani
Kwa upande wake Mbunge wa kuteuliwa Riziki Lulida aliwashukuru wananchi waliojitokeza kujumuika nae kwenye tukio hilo muhimu la kupata futari ya pamoja kwani kufanikiwa kwa ghafla hiyo kumetokana na ujio wao.
Alisema ameamua kupata futari ya pamoja na makundi hayo maalumu ili kuwa pamoja na ndugu zake wana Lindi katika kumshukuru mwenyezimungu sambamba na kumcha mwenyezimungu
Pia mama Lulida pamoja na kupata futari hiyo aliwakumbusha waislamu wenzie juu ya umuhimu wa swala, kutoa dhaka kwa wenyeuwezo , kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja na kufanya ibada ya hija.
Akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa wa Lindi , Mkurugenzi wa Mnispaa ya Lindi Bw. Juma Mnwele pamoja na kumpongeza mbunge huyo kwa kuwakumbuka na kuwathamini watu hao wa makundi maalumu kwa kupata nao futari ya pamoja pia aliwataka waislamu na wakazi wa mji wa Lindi kwa ujumla kuendelea kuuombea mkoa huo wa Lindi pamoja na viongozi wa mkoa na Taifa .
0 Comments