Header Ads Widget

ASKOFU KKKT IRINGA DKT GAVILE ,AKEMEA USHOGA AONESHA NJIA YA UKOSEFU WA AJIRA NCHINI

 



Na  Matukio Daima App,Iringa

ASKOFU wa  kanisa la  kiinjili la  kilutheri Tanzania (KKKT)  dayosisi ya  Iringa  Dkt  Blaston Gavile (pichani)amesema  suala la ajira  kwa  sasa  limekuwa ni changamoto  kubwa  serikalini  hivyo  njia  pekee ya  kupambana na tatizo la  ajira  ni vema  kila  moja  kujiajili katika  sekta  binafsi .

 

Alisema  kuwa  badala  ya  kutegemea  ajira   kutoka  serikali  ni  vema  kila mmoja  kufanya kazi  kupitia  sekta  binafsi kama  kilimo cha Parachichi , ufugaji na  nyingine  nyingi.

 

Alisema  suala la  ajira  kwa  sasa  limekuwa ni  gumu  zaidi  kutokana na  uhitaji wa ajira  kuwa mkubwa  na  serikali haiwezi  kuajiri kila mmoja  wetu .

 

Pamoja na  kutoa  wito  wa  kila mtanzania   kuacha  kutegemea ajira  serikali  askofu  Dkt  Gavile  awataka  waumini  wa kanisa  hilo na watanzania kwa  ujumla  kuendelea  kuliombea  Taifa  na  viongozi wote akiwemo Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan  ili kuliongoza Taifa katika  misingi bora  inayozingatia  katiba na utawala  bora .

 

Askofu  Dkt Gavile alitoa  wito  huo Leo   wakati  akitoa   salam  za Pasaka kwa  waumini  wa Dayosisi ya Iringa katika  ibada   iliyofanyika  usharika  wa Kanisa  kuu Iringa .

 

Kuhusu  mmomonyoko  wa  maadili  alisema  kuwa  hali halisi ya mmomonyoko wa  maadili ndani ya  mkoa wa Iringa na Taifa  si njema  kwani kila  siku  matukio ya  ulawiti ,ushoga na usagaji yameendelea  kuripotiwa  jambo ambalo halikubaliki katika jamii .

 

“ Kazi yetu sisi wa Kristo ni  kukemea  vitendo   hivyo visivyompendeza Mungu  na  kuomba toba   ili  aturehemu kuondokana na mambo hayo yasiyompendeza  Mungu ukisoma  Mwanzo  sura  ile ya 18 hadi 19  inaeleza   jinsi ambavyo Ibrahimu  alivyoomba toba  kwa  ajiri  ya  Sodoma na Gomola ambao  waliadhibiwa  kwa  ajili ya  Dhambi  lakini  nae  Ibrahim  alizidi  kusimama katika  Bwana  “

 

Alisema  pamoja na  kumuomba  Mungu  bado wazazi na jamii inawajibu  wa  kuendelea  kuongeza  ulinzi kwa  Watoto  ili nao  waweze  kutimiza  ndoto na malengo yao .

Mafundisho ya  Uzushi  kuwa  siku  hizo  kumeendelea  kuibuka mafundisho ya uzushi   ambayo yanakaza  zaidi mafanikio ya  kiuchumi  pasipo  kufanya kazi na kuelekea  watu  kutangatanga  kutafuta mahubiri hayo ambayo mwisho wa  siku  yanawapeleka  kubaya  zaidi .

 

Alisema hakuna  mafaniko  pasipo  kufanya kazi  hivyo ni  vema  kila mmoja  kutambua mafaniko ya kweli ni kufanya kazi sio kutegemea  wazushi na  wapotoshaji wa maandiko ya Mungu .

 

Aidha  Askofu  Dkt  Gavile  aliwataka  waumini wa kanisa  hilo wanaposherekea  sikukuu ya Pasak ana  wakati  wote  kuendelea  kuomba kwa  ajili ya viongozi  wa nchi  akiwemo Rais , makamu wa Rais , waziri mkuu na  spika  wa Bunge  ili  waongozi  nchi vema .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI