NA HADIJA OMARY
LINDI
MTOTO mchanga wa kike anaekadiliwa kuwa na umri wa mwezi mmoja na nusu tangu azalipozaliwa ,ambaye hajafahamika alikotokea,ametelelelekezwa na mama yeke na kutokomea kusikojulikana na kuokotwa na wasamalia wema
Kichanga hicho kilichopewa jina la Enjo ameokotwa na Rehema Ally Sina-uwanja,pembezoni mwa Nyumba anayoishi iliyopo mtaa na barabara ya Kawawa,karibu na kituo cha Mafuta cha Buti la Zungu, machi 30 mwaka huu majira ya saa 2:00 usiku.
Sina-uwanja akielezea namna alivyomuokota kichanga hicho mbele ya mwandishi wa Habari hizi,amesema siku hiyo akiwa ndani ya Nyumba anayoishi akiendelea na kazi yake ya kushona nguo,alisikia sauti ya Mtoto mchanga akilia bila ya kubembelezwa na mtu aliyekuwa nae.
Amesema kilio hicho kilichochukuwa muda mrefu,kilimstua mno na kulazimika atoke nje na kwenda Nyumba kubwa kuwaita wapangaji wenzake waelekee anakolia Mtoto huyo kutambua kama yupo na mtu au peke yake ametupwa.
“Nilipofungua mlango namkuta mtoto Pembezoni mwa ukuta wa Nyumba tunayoishi kimeveshwa suweta kubwa na kutandikiwa nguo aina ya Dera na kichwani kawekewa mtandio kitambaa”Alisema Sina-uwanja.
Sina-uwanja amesema baada ya wapangaji wenzake kujitokeza akiwemo Juma Kilole au baba Nadia na kukiona kichanga hicho,wakatoa taarifa kwa mwenyekiti wa Mtaa wao,Hadija Selemani na kumchukuwa kwendanae Kituo cha Polisi Wilaya kilichopo mjini Lindi.
Alisema baada ya kufika kituo cha Polisi walielezwa na askari wa zamu waliowakuta wampeleke Mtoto huyo Hospitali ya Sokoie,kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu kufahamu hali ya Afya yake,kama ipo salama au imehathiriwa na kitendo cha kutelekezwa kwake.
Pia,amewaomba wanawake wenzake kuacha tabia ya kutupa watoto wanaowazaa,kwani kufanya hivyo,wanamkosea mwenyezi-mungu anaowapa riziki zinazotokana na kupewa mimba na wanaume kisha kuwakataa,badala yake waendelee kuwalea kwani aseti kwa maisha yao ya baadae watakapoishiwa nguvu.
Mganga mfawidhi Hospitali ya Sokoine,mkoani Lindi,Dr Alexander Makalla alipofuatwa kumuulizia swala la kichanga hicho,amethibitisha kumpokea Mtoto huyo aliyeeleza ana uzito wa kilo tatu na kukifanyia uchunguzi wa kitaalamu na kubaini yupo na Afya njema bila shida.
“Ni kweli kichanga hicho kimefikishwa kwetu hapa machi 30/2023 saa 4:00 usiku,tumekifanyia uchunguzi wa kitaalamu tumekibaini kutokuwa na tatizo lolote la Afya”Alisema Dr Makalla.
Dr Makalla amesema baada ya uchunguzi huo wa kitaalamu kichanga hicho kimebainika kutokuwa na madhara ya ki-afya na kukabidhiwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Sokoine, Rufoya Kassimu kwa taratibu zingine namna za kumtunza Mtoto huyo.
Kassimu alipofuatwa na mwandishi wa Habari hizi,amekiri kukabidhiwa kichanga hicho na kueleza tayari ameshakabidhi kwa Afisa Ustawi mwenzake wa Manispaa ya Lindi, Richard Kimaro.
Afisa Ustawi wa Manispaa ya Lindi, Richard Kimaro alipoulizwa na mwandishi wa Habari hizi,amethibitisha kukabidhiwa mtoto huyo na yeye kukabidhi kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalum kiitwacho Loving Heart Caring Hands kilichopo kata ya Jamhuri mjini Lindi.
Mkurugenzi wa Kituo cha Loving Heart Caring Hands,Mohamedi Chigogoro alipofuatwa na mwandishi wa Habari hizi,amekiri kumpokea mtoto huyo Apriri 04 mwaka huu,kutokea kwa Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Lindi, Richard Kimaro.
Chigogoro amesema huyo ni Mtoto wa pili kupokelewa na Kituo hicho mwaka huu,kwani hivi karibuni wamepokea mtoto wa kiume akitokea Wilaya ya Masasi,Mkoani Mtwara na kufanya kiwe na idadi ya watoto wanne wanaoishi na kulelewa hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Lindi,Pilli Mande alipoulizwa kupitia simu yake ya mkononi,kama taarifa ya kuokotwa kwa kichanga hicho imeshafikishwa mezani kwake,alijibu kwa kusema bado hajaiona,kwani yupo safarini kikazi Wilaya ya Liwale.
MWISHO.
0 Comments