Header Ads Widget

ASKOFU DKT MPELI ATAKA WALIOTAJWA RIPOTI YA CAG WAREJESHE FEDHA

 


ASKOFU  wa kanisa  la  ACTS Felloshp Tanzania  DKt  Mpeli  Mwaisumbe amesema  kazi  inayofanywa na  Rais  Dkt  Samia  Suluhu  Hassan katika  Taifa  ni  kubwa  na  utendaji  wake  unajidhihilisha  kuwa ni Rais bora Mwanamke Afrika  hivyo  jukumu la  watanzania  kuendelea  kumuombea  ili  azidi  kuliongoza  Taifa  vema   huku  akimuomba kutowaonea  haya   vigogo  wote   waliotajwa  kwenye  ripoti ya mdhibiti na mkaguzi wa  hesabu  za  serikali (CAG).

Akitoa  salam  za Pasaka leo  mara baada ya  ibada  katika  kanisa la ACTS  Felloship Centre  Iringa mjini  Dkt  Mwaisumnbe  alisema  kuwa  mbali ya  Taifa  kuendelea  kujivunia mafanikio makubwa ambayo yameletwa na  serikali ya awamu ya  sita  chini ya Rais  Dkt  Samia  ,ila  bado kuna mambo  ambayo  yanakwenda  ndivyo  sivyo na  kila mmoja anawajibu wa  kukemea kwa  nguvu  zote .

Kuwa  hivi karibuni imetoka  ripoti ya CAG  na katika  ripoti  hiyo kuna  watu  wametajwa  kuhusika na matumizi mabaya ya  fedfha  za  umma  fedha  ambazo  kama  zingetumika  vizuri  zingesaidia   kuleta maendeleo  kwenye  Taifa   hivyo bila  kuangalia  sura ya   kiongozi ni  vizuri  fedha    hizo  zikarejeshwa  ili  zielekezwe  kwenye miradi ya maendeleo .

" Mheshimiwa  Rais wetu  mama  Dkt  Samia Suluhu  Hassan  amekuwa mfano  mwema  wa uongozi  kwenye  Taifa na hata  bara  zima la Afrika  hivyo  tunahitaji  kumuunga mkono wote  kwa  nguvu  zetu  zote sisi   viongozi wa  dini tuendelee  kumuombea afya  njema  ila  na wale  waliopo  serikalini   wanaomsaidia  wawe  waadilifu wa  fedha za umma"  alisema  askofu Dkt  Mpeli .



Akizungumzia  kuhusu  maadili katika  jamii askofu Dkt  Mpeli alisema  ni  wajibu wa jamii kuendelea  kukemea  vitendo vya ushoga na  usagaji  vinavyoendelea  kuchipua katika  jamii kwani  vitendo  hivyo ni  chukizo mbele za Mungu na kila  mzazi ama mlezi anawajibu  wa  kutoa  elimu kwa   watoto  wake  ili  kuepukana na vitendo  viovu vya  ndoa  za jinsia moja .

Alisema  Yesu  Kristo alibeba   dhambi  zetu na hata  kufa msalabani kwa  ajili  ya  wote  wenye  dhambi  hivyo wakati  wakristo  kote  ulimwenguni wanaposherekea  sikukuu ya   kufufuka kwake  Yesu  Kristo ni vema  kuachana na mambo  yote maovu  yasiyompendeza  Mungu ili  Yesu kristo  afufuke ndani ya  mioyo na sio katika mavazi ama chakula .















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI