NA HADIJA OMARY
LINDI
Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka serikali kupitia Wizara ya Nishati kuhakikisha rasilimali zinazotokana ujio wa mradi wa uchakataji wa Gesi asilia LNG unaotarajia kutekelezwa katika Manispaa ya Lindi Mkoani humo unaanze kuwanufaisha wananchi wa Mkoa huo kiuchumi ikiwa pamoja na manispaa hiyo kuwa mwanahisa wa mradi huo.
Rai hiyo imetolewa na kiongozi wa chama hiko Zitto Zuber Kabwe jana alipokuwa anazungumza na Wananchi katika viwanja vya Shule ya msingi Mpilipili manispaa ya Lindi Mkoani humo wakati wa Uzinduzi wa Mikutano ya Adhara ya chama hiko.
Zitto alisema kuwa chama hiko kinataka rasilimali ya Gesi kwa wote kwa maslahi ya wote sio Gesi hiyo iendelee kunufaisha maeneo mengine na kuubakiza Mkoa huo wa Lindi ukiwa Nyuma. Hivyo serikali kupitia wizara ya Nishati ni lazima iwe na mpango maalumu wa kuhakikisha mradi huo unawanifaisha wana Lindi na Watanzania kwa ujumla
alisema miongoni mwa mambo ambayo yanatakiwa kufanyika wakati wa utekelezaji wa Mradi huo ili wana Lindi waweze kunufaika ni pamoja na manispaa ya hiyo kwa niaba ya Wananchi lazima iwe na hisa angalau kwa asilimia 2.5% ya thamani ya mradi mzima.
“kuna kitu wataalam wanaita (Land for equity) Aridhi kama mtaji, ile Aridhi ambayo watajengea mradi ndio hapa manispaa ya Lindi iwe mtaji wao ili fedha zitakazopatikana zitumike kwa ajili ya watu wa Lindi.
Jambo linguine ni kuitaka serikali kuandaa mpango kabambe wa jiji la Lindi ambao utaangazia muktadha wa mradi huo Mkubwa wa uchakataji wa Gesi Asilia ili kulinda maslahi ya watu wa Lindi.
Nae katibu Mkuu wa chama hiko ndugu Ado Shaibu Ado alisema wanaipongeza serikali kwa kuharakisha mazungumzo na wawekezaji wa Mradi huo ambayo yalikuwa yamekwama kwa miaka takribani mitano iliyopita .
“mradi huo wenye thamani ya tilioni 70 ukikamilika vizuri unaweza kuleta manufaa makubwa , kwa wana Lindi na Watanzania kwa ujumla, changamoto ni kwamba hatuoni Mpango wowote wa Serikali kuhakikisha kwamba wananchi wa Lindi na watanzania kwa ujumla wananufaika ipasavyo na mradi huo “ alisisitiza Ado
0 Comments