Header Ads Widget

WANAWAKE MADEREVA MBIO I KUANZISHA CHAMA CHAO

 


CHAMA Cha Madereva Wanawake Tanzania (CWMT) kinatarajia kuanzisha kampuni ya usafirishaji ili kujiongezea kipato na kutoa ajira kwa wanachama wake.


Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa chama hicho Naetwe Ihema alisema kuwa lengo ni kumkwamua mwanamke ili ajitegemee na asiwe tegemezi.


Ihema alisema kuwa madereva wanawake kwa sasa ni wengi ambao wanafanya kazi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye Taasisi za serikali na binafsi lakini walikuwa hawana Umoja wao.


"Tumeanzisha chama hichi ambacho mwanzo ilikuwa ni kikundi tukaona tujiongeza na kuwa chama ambacho kimesajiliwa na moja ya malengo yetu ni kuwa na kampuni ya usafirishaji kwa mabasi ya kwenda mikoani na daladala ambapo wanachama wetu watakuwa ndiyo madereva,"alisema Ihema.                     Aliongeza kuwa sifa ya mwanachama awe anaendesha chombo chochote cha moto ambapo baadhi ya wanachama wao ni marubani wa ndege, manahodha wa meli, madereva wa mitambo ya ujenzi, magari ya mizigo, mabasi makubwa, madereva wa treni, madereva wa uba, madereva wa mwendokasi na magari ya watu binafsi. Chama hicho kilianzishwa mwaka 2020 na kina wanachama 120.     


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI