Header Ads Widget

WATAALAM WA AFYA MKOANI TANGA WAPEWA MAFUNZO

 


Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP Tanga. 


Wataalam wa Afya toka Halmashauri 11 Mkoani Tanga wametakiwa kusimamia ukusanyaji wa mapato katika vituo vya kutolea huduma ya Afya ili waweze kuwalipa Washitiri kwa wakati baada ya kupokea shehena ya bidhaa za afya na kuepuka madeni yasiyoyalazima.


Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga George Mmbaga wakati wa mafunzo yanayotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(tamisemi)yanayohusu mfumo wa kieletroniki wa ugavi wa bidhaa za afya.


Mmbaga alisema kuwepo kwa Washitiri (wachuuzi wabobezi) ni utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020 ambayo inataka hospitali zote Nchini zihakikishe zinakuwa na dawa hivyo bohari za dawa (msd) zinapopungukiwa au kutokuwa na dawa na vifaa tiba lazima kuwepo na wasambazaji wengine watakaotoa huduma hiyo.


Aidha alisema mfumo huo  utarahisisha upatikanaji wa bidhaa za Afya zitakazokosekana katika bohari za madawa (msd) ili kuimarisha na kurahisisha upatikanaji wa bidhaa hizo katika vituo vya kutolea huduma za afya Nchini jambo ambalo limekuwa ni changamoto.


"Ninaimani washiriki baada ya mafunzo haya wote mtaondoka na uwelewa wa pamoja wa utekelezaji wa muongozo wa mfumo huo ili uweze kusimamia kikamilifu na kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanakamilika"Alisema Mmbaga.



Hata hivyo alisema ili mfumo huo uwe bora maafisa hao wa Afya wametakiwa kusimamia vema kuanzia utaratibu wa awali wa upatikanaji wa washitiri na utekelezaji wao wa kimkataba na mtambue umakini wenu ndio chanzo cha kutimiza malengo ya kupatikana kwa dawa kwa urahisi.


"Na niwaombe kila mmoja akatimize wajibu wake na ahakikishe shughuli zote za washitiri zinatekelezwa kwa mujibu wa muongozo'Alisema Mmbaga.


Kwa upande wake Mfamasia msaidizi Mkoa Tanga Beata Kimaro alisema takriban washiriki 100 katika vitengo vya ufamasia,manunuzi,it na wataalam wa maabara toka Halmashauri zote Mkoani hapa  wamepatiwa elimu ya mfumo maalum wa kutathimini utendaji wa kazi za washitiri kwa njia ya eletronik.


Kimaro alisema wawezeshwaji ni kutoka ngazi ya Wilaya na Halmashauri ili wao waweze kwenda kufundisha ngazi za Chini, zahanati na vituo vya afya ili kuweza kumsimamia mshitiri ufanyaji wa kazi zake kupitia mfumo huo katika ngazi zote kuanzia Taifa hadi Halmashauri tofauti na hapo awali.



Alisema mfumo huo wa kieletroniki unauwezo wa kuona taarifa kwa haraka za ufanyaji kazi wa mshitiri na kubaini uwezo wake wa kutimiza mahitaji ambayo vituo ama zahanati yaliyopelekwa kwake na kubaini tarehe ya maombi na utekelezaji wake.


"Huu mfumo utatusaidia sana maana hapo awali tulipata shida kutokana na tulikuwa na mifumo isiyo rafiki lakini sasa ni rahisi tunauwezo wa kuona maombi yote,ucheleweshwaji uko wapi na ni rahisi kubaini kila kitu na kuchukua hatua za haraka"Alisema Kimaro.


Nae Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Rehema Majid alisema mfumo huu utakuwa na tija kwa wananchi kutokana na kuwepo kwa upatikanaji wa dawa kwa urahisi ikiwa bohari za dawa hazitokuwa na bidhaa za afya huduma hiyo itatolewa na washitiri ambao watakuwa wasambazaji mbadala.



Hata hivyo alisema matumaini kwa washiriki hao ni kuona wana kwenda kutumia mfumo huo wa kisasa zaidi na kwenda kutoa elimu hiyo katika maeneo yao na kuweza kuwasimamia vema washitiri ili huduma itolewe kwa wakati kama ilivyokusudiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI