NA MATUKIO DAIMA APP.
DAR ES SALAAM.Meneja wa Wakala wa Barabara za vijijini na mijini TARURA mkoa wa Dar es Salaam Eng. Geofrey Mkinga amevitaka vikundi maalumu vya Wakandarasi wa nguvu kazi stahiki kuchangamkia kufanya manunuzi ya kazi za Wakala hao mkoa huo kwani Kuna zaidi ya billioni 15 kwa utekelezaji wa kazi hizo mwaka huu.
Amesema hayo ofisini kwake wakati akizungumza na Wakandalasi wa vikundi maalumu vya ukandarasi vya nguvu kazi stahiki wa mkoa huo ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 na kanuni za mwaka 2024 zinataka taasisi za manunuzi kutenga angalau 30% ya bajeti ya ununuzi kwa makundi maalumu hayo.
Amesema bajeti ya TARURA mkoa wa Dar es Salaam hutenga zaidi ya Shilingi bilioni 50 ambapo bilioni 15 ni kwaajili ya vikundi maalum vya ukandarasi vya nguvu kazi stahiki lakini katika kipindi cha bajeti za kati ya mwaka 2022 hadi mwaka 2025 huishia kuchukua kiasi cha Shilingi milioni 300 ndicho kilitumiwa na vikundi hivyo Kila mwaka.
"Vikundi maalum hivyo kwa kuto kufanya manunuzi kazi za Wakala hao katika mfumo wa NEST kwasababu mbalimbali husababisha baadhi ya miradi kutotekelezwa mkoani humo" alisema Eng. Mkinga.
Amesema Tanzania nzima kuna vikundi 597 vimejisajili katika mfumo wa NEST lakini ni vikundi kumi tu ndio vilivyojisajili katika mkoa wa Dar es Salaam lakini hatahivyo vikundi hivyo kumi haviombi kazi hizo katika mkoa huo.
Alizitaja baadhi ya miradi inayotakiwa kufanywa na vikundi maalum hivyo ikiwa ni kwa takwa la kisheria kuwa ni pamoja na kufanya ununuzi na usimamizi wa mikataba ya usanifu, matengenezo, matengenezo ya dharura, maboresho, ukarabati na ujenzi wa Barabara.
Eng. Mkinga amesema wameamua kukutana na Wakandalasi hao ili kuwahamasisha na kusikiliza changamoto wanazokutana nazo katika kufanya manunuzi ya kazi za Wakala hao katika mkoa huo na kuzitafutia ufumbuzi ili takwa hilo la kisheria litekeleseke na makundi hayo mkoani humo.
"Sisi tupo tayari kushirikiana na nyinyi ili lengo na madhumuni ya serikali kutenga 30% ya fedha kwaajili ya kundi hilo litatekelezeka""
"Tumesikia mitazamo yenu na changamoto zenu ambazo hasa kuhusu mashariti ya ushirikiano wenu kikamilifu" Alisema Eng. Mkinga.
Akizungumzia changamoto za kimfumo wa NEST aliahidi kushughulikia kupitia wataalamu wao.
Aidha amewataka kupitia vizuri miongozo ili kujua wajibu na mashariti ya utendaji kazi wao baina yao na Wakala hao na serikali ili dhamila ya serikali kutenga Sheria hiyo litimie kwa maendeleo endelevu ya mwananchi mmoja mmoja na taifa lote kwa ujumla.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo Mama Mate Kamba aliomba Wakandalasi hao kukopesheka kupitia fedha za halmashauri kwani miradi hiyo unauhakika wa kurejeshwa kutokana na mikataba yake na serikali.
+++++
0 Comments