Header Ads Widget

WATAKIWA KUSAJILI MAJINA YA BIASHARA BRELA.

WAMILIKI wa makampuni na biashara Jiji la Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza kupata huduma ya kusajili majina ya biashara zao ili ziwe kisheria.

Hayo yalisemwa na Msaidizi wa Usajili wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Yvonne Maselle wakati wa maonyesho ya wajasiriamali na wafanyabiashara yanafanyika kwenye viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.


Maselle alisema kuwa Brela ni miongoni mwa mabanda ya taasisi za serikali yanayotoa huduma kwenye maonyesho hayo ambapo wanahamasisha wafanyabiashara wasajili majina ya biashara zao.


"Tunamshukuru Mungu kwa mwitikio huu waliouonyesha japo itakuwa ni vigumu kwa sasa kutoa idadi ya waliojisajili kama unavyoona wamejitokeza lakini bado tunawahamasisha waje kwa wingi,"alisema Maselle.


Alisema kuwa  Brela inaamini siku za mapumziko ambazo ni Jumamosi na Jumapili wafanyabiashara wengi watafika kupata huduma ya usajili.

"Tumejipanga vyema kuwahudumia kwani mbali na  kujisaliji  tumekua tukitoa ushauri kwa mteja mmoja mmoja ili waweze kupata ufahamu zaidi ya kujisajili,"alisema.


Aidha alisema kuwa wanatoa huduma ya usajili wa kampuni, majina ya biashara, alama za biashara na leseni za viwanda.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI