Header Ads Widget

TAKUKURU MWANZA YABAINI MAPUNGUFU KATIKA MIRADI 22

 


NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA


Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza imebaini mapungufu katika miradi 22 yenye thamani ya sh 6,538,933,062.49.


Hayo yamebainishwa na Mkuu wa TAKUKURU James Ruge wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu Katika kipindi Cha miezi mitatu kuanzia oktoba mwaka 2022 Hadi Disemba 2022.


Ruge amebainisha miradi iliyokutwa na  mapungufu ni sekta ya afya, sekta ya maji pamoja na sekta ya  elimu jumla ya vyumba 92 vya madarasa katika shule 12 za Halmashauri ya Jiji Mwanza.


Ametaja shule zilizo na mapungufu katika Miradi hiyo ikiwa ni pamoja na shamaliwa madarasa 10 yenye thamani ya sh 260,000,000, igoma madarasa 10 yenye thamani ya sh 200,000,000, mahina madarasa 9 yenye thamani ya sh 220,000,000, Buhongwa madarasa 12 yenye thamani ya sh 330,000,000, Capri point madarasa 8 yenye thamani ya sh 220,000,000, 


Bugarika madarasa 4 yenye thamani ya sh, 120,000,000, Mkolani madarasa 11 yenye thamani ya sh, 120,000,000, Mlimani madarasa 4 yenye thamani ya sh, 120,000,000, Mtoni madarasa 10 yenye thamani ya sh 360,000,000, Mhandu madarasa 9 yenye thamani ya sh 220,000,000.


Ameeleza kuwa wameendelea kutekeleza jukumu la uelemishaji wa umma Kwa lengo la kuwashirikisha wananchi kwenye mapambano dhidi ya Rushwa.


" Katika kutekeleza la kuelimisha umma katika kuadhimisha wiki na siku ya maadili, TAKUKURU Kwa kushirikiana na ofisi ya sekretarieti ya maadili ya uongozi wa umma wameendelea kutoa elimu Kwa lengo la kuhimiza watumishi na wananchi kuzingatia maadili katika utoaji na upatikanaji huduma za za utekelezaji Wa miradi ya Maendeleo Alisema Ruge".


Ruge amebainisha mikakati ya robo ya tatu ya mwaka 2022/2023 ni pamoja na kutatua kero mbalimbali katika jamii kupitia programu ya TAKUKURU rafiki, kuzuia vitendo vya Rushwa katika utekelezaji wa Maendeleo, kutoa elimu ya mapambano dhidi ya Rushwa,kuchunguza makosa ya Rushwa Kwa wale watakaobainika.


Aidha amewataka wananchi kuendelea kufuatilia elimu ya makosa ya rushwa Kwa mujibu wa sheria pamoja na majukumu ya TAKUKURU Kwa mjibu wa sheria.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI