Header Ads Widget

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUKABILI UGONJWA WA KIFUA KIKUU

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


SERIKALI imedhamiria kuendelea kushirikiana na wadau katika sekta zote ili kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ifikapo mwaka 2030.


Hayo yamesemwa na Katibu  Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi katika  kikao na Makatibu Wakuu wa Wizara kilichofanyika katika ofisi za Waziri Mkuu Jijini Dodoma.


“Ili kudhibiti ugonjwa huu wa Kifua Kikuu ni muhimu kushirikiana na wadau wengi kama sekta ya afya, wadau sekta ya elimu, sekta ya usafirishaji na sekta nyingine mbalimbali.” amesema Dkt. Yonazi.


Kwa upande wake Mtaalamu Mshauri kutoka Stop TB Partnership (STP)  Oscar Mukasa wakati akiwasilisha taarifa ya mpango kazi wa kudhibiti Kifua Kikuu amesema watu wenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo  ni pamoja na watu wanaoishi katika  makazi duni, Watoto, Wavuvi na  wanafunzi wanaoishi bweni.



“Kuna makundi mengine  ambayo yako hatarini kupata maambukizi Watu wenye VVU, watu wenye Utapiamlo, wachimbaji madini, wanaoishi na mgonjwa wa Kifua Kikuu, watoa huduma za afya na wanaotumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano,” Ameeleza Mshauri huyo


Aidha  Mukasa amewashauri wanaoishi katika mazingira hayo kuchukua tahadhari  za kujikinga na ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB).


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI