Na Pamela Mollel,Arusha
Mamlaka ya hifadhi za Taifa Tanzania kupitia Hifadhi ya Arusha imekabidhi miradi ya maendeleo yenye thamani ya Milioni 322,705,325 ikiwemo mradi wa Zahanati mpya ya ILkurumi pamoja na vifaa tiba kwa wakazi wa kata ya Ngarenanyuki Wilayani Arumeru Mkoani Arusha
Akizungumza katika Hafla ya kukabidhi miradi hiyo iliyowezeshwa kwa ushirikiano wa Tanapa na wananchi Kaimu Mkuu wa Uhifadhi PCO Maria Saidia alisema kupitia mradi huo wa ujirani mwema kwa vijijini ambayo vinapakana na hifadhi ya Arusha wameweza kufanikisha miradi hiyo
Alitaja miradi hiyo kuwa ni kuwezesha ununuzi wa viti 90 meza 90 za wanafunzi pamoja na meza nne na viti vinne kwaajili ya waalimu wa shule ya Sekondari Losinoni,ujenzi wa ukuta wa uzio mita 50 katika shule ya sekondari Kisimiri
Alisema mbali na vifaa hivyo pia waliwezesha ununuzi wa vifaa tiba na samani katika Zahanati ya ILikuruki kata ya ngarenanyuki,madawati 60 kwa shule ya msingi Olkung'wado pamoja na ununuzi wa mizinga 200 na vifaa vya kurinia Asali kwa vikundi vinne vilivyopo katika vijiji vya Leguruki na Ngurudoto
Aidha aliongeza kuwa Shirika hilo lina utaratibu wa kuunga mkono jitihada za wananchi kwa kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo na kijamii sambamba na utunzaji wa mazingira
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo ambaye alimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Arumeru,Sangai Laizer ambaye ni Afisa Tarafa ya King'ori aliwapongeza Tanapa pamoja na wananchi kushirikiana kwa pamoja katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Pia aliwataka wananchi hao kuitunza na kuithamini miradi hiyo ili iweze kusaidia wananchi kama ilivyokusudiwa
"Kina baba na mama zangu hii miradi ni muhimu sanaa na imegharimu fedha nyingi sanaaa za serikali hebu tuingalie hii miradi kwa jicho la pekee"alisema Laizer
Aidha aliwakumbusha wananchi hao juu ya umuhimu wa kutunza mazingira na wanyama kwaajili ya vizazi vijavyo
0 Comments