Na Fadhili Abdallah,Kigoma
POLISI mkoani Kigoma ikiongozwa na Kamanda wa polisi wa mkoa huo Filemon Makungu imevamia kituo kikuu cha mabasi mkoani Kigoma kufanya ukaguzi na kuzungumza na madereva wa mabasi yanayofanya safari nje ya mkoa.
Akizungumza na madereva wa mabasi ya abiria na abiria waliokuwa wakisafiri na mabasi hiyo Kamanda Makungu alisema kuwa ajali nyingi za barabarani zina epukika na kubainisha kuwa uzembe wa madereva ndiyo chanzo kikuu cha ajali hizo.
Kamanda Makungu alitaja vyanzo vikubwa vya ajali kuwa ni ulevi wa madereva, mwendo kas usiozingatia taratibu za usalama, ubovu wa gari unaojulikana na kuendesha gari mwendo mrefu huku dereva akiwa peke yake.
Alisema kuwa wakati huu wa wiki ya usalama barabarani polisi imejapanga kuhakikisha inafanya ukaguzi na kuchukua hatua kwa madereva na wamiliki wa magari ambao hawazingatii taratibu za usalama barabara zinazosababisha ajali.
Kwa upande wake Mkuu wa usalama barabarani mkoa Kigoma, Timoth Chikoti alisema kuwa abiria wanayo nafasi kubwa ya kuzuia ajali za barabara kwenye mabasi ya abiria kwa kutoa taarifa kuhusu mwendo kasi au ubovu wa magari ili polisi waweze kuchukua hatua.
Akizingumza mbele ya Kamanda wa polisi mkoa Kigoma Dereva wa basi la Adventure linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Kigoma, Jumanne Salim alisema kuwa wenye magari makubwa (malori) chanzo cha ajali nyingi za barabarani.
Alisema kuwa pamoja na kudhibitiwa kwa mabari ya abiria lakini alitaka wenye malori ambayo yanabeba mizigo mikubwa kwa sababu wanaendesha kwa namna ambayo imekuwa ikileta usumbufu kwa magari mengine na kusababisha.
0 Comments