Header Ads Widget

DKT. KIRUSWA AELEZA MAFANIKIO YA DHANA YA USHIRIKISHWAJI SEKTA YA MADINI, AJIRA ZA ONGEZEKA HADI KUFIKIA 15,341.

 



NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA


Naibu waziri wa madini Dkt Steven Kiruswa amesema kuwa ajira sekta ya madini imeongezeka kutoka 6668 ya mwaka 2018 na kufikia 15341 ya mwaka 2022 kwenye migodi mikubwa ambapo mafanikio hayo ni sehemu ya ushirikishwaji wa watanzania katika sekta hiyo.


Dkt Kiruswa aliyasema hayo wakati akifungua jukwa la pili la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini ambapo alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo pia katika nafasi zinazohitaji uzoefu kutokana na ukuaji wa teknolojia kumekuwa na utaratibu wa kisheria wa urithishwaji watanzania kwa nafasi zinazoshikiliwa na wageni.



Alisema kwa  kipindi cha mwaka 2018 hadi 2022 jumla ya watanzania 8066 wamepatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo katika utendaji kazi ambapo jumla ya shilingi bilioni 3.4 zilitumika ili kuwawezesha kufanya kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na wageni.



Aidha alisema wizara kupitia time ya madini imeendelea kusimamamia manunuzi ya bidhaa na huduma kwa kuhakikisha kipaumbele kinatolewa kwa watanzania ambapo usimamizi huo umekuwa na matokeo chanya kwa kuongeza idadi ya watanzania watoa huduma na kuuza kwanzia migodini, wachimbaji wadogo na wakubwa katika sehemu zote zenye madini nchini.



“2022 jumla ya Dola za kimarekani billion 2.2 sawa na asilimia 97.4 ya manunuzi ya makampuni ya yote ya madini yalifanyika kwa kutumia kampuni za watanzania ambapo pia ongezeko la watoa huduma kwa mwaka 2021 wamefikia 1386 sawa na asilimia 81 ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo kulikuwa na watoa huduma 623 tu,”Alisema Dkt Kiruswa.


Sambamba na hayo akizindua  mfumo wa ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content) na wa utoaji wa huduma kwenye jamii unaofanywa na migodi ya madini (CSR) iliyofanyika katika jukwaa hilo Dkt Kiruswa alisema kuwa mfumo utawezesha kampuni za uchimbaji wa madini na watoa huduma kwenye migodi ya madini kuwasilisha nyaraka mbalimbali kwenye uwasilishaji wa mipango ya ushirikishwaji wa watanzania katika  Sekta ya Madini na utoaji wa huduma kwa jamii kwenye migodi ya madini kwa njia ya kieletroniki badala ya kutumia nakala ngumu kama ilivyokuwa ikifanyika awali.




Kwa upande wake  kamishna wa Tume ya Madini, Janet Lekashingo ameongeza kuwa Serikali kupitia Tume ya Madini bado inaendelea kutoa elimu  katika mikoa mbalimbali nchini kuhusu ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini  ili wananchi wengi waweze kushiriki kwenye shughuli za utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI