Header Ads Widget

BILIONI 12.86 ZAHITAJIKA KUKAMILISHA KIWANDA CHA GLAVU MAKAMBAKO NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Kiasi Cha shilingi bilioni 12.86 kinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa kiwanda Cha Dawa kilichopo Idofi Makambako mkoani Njombe ambacho kinatarajia kuanza uzalishaji ifikapo mwezi Julai mwaka huu.


Aidha kiasi Cha shilingi Bilioni 16 zimeshatumika mpaka sasa kujenga kiwanda hicho na mpaka kukamilika kwake kitagharimu shilingi bilioni 21.



Mkurugenzi  mkuu wa  bohari ya Dawa nchini Mavere Tukai amesema  Bajeti imekuwa changamoto kubwa ya kukamilisha ujenzi wa kiwanda hicho hasa kufikia hatua ya mwisho.


Makamu mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali Japhet Hasunga Mbunge wa Jimbo la Vwawa kwa niaba ya Kamati ya bunge amekiri kupokea maombi ya kiwanda hicho na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi.



Wakazi wa Idofi Makambako akiwemo Magdalena Nduya na Mexon Kibiki wanatumia fursa hiyo kuiomba Serikali ikamilishe ujenzi huo na kianze kutoa Huduma ili wanufaike na uwepo wake.



Kwa Upande wake mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Bohari ya Dawa MSD Rosemary Silaa amesema licha ya kutarajia kuanza kuzalisha mipira katika kiwanda hicho lakini kitazalisha ajira hadi kwa wakulima wa zao la mpira.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI