Header Ads Widget

DC NJOMBE: AAGIZA WAJASIRIAMALI WAPEWE MIKOPO MIKUBWA

 



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ameziagiza halmashauri zote tatu za wilaya yake kuanza kutoa mikopo mikubwa kwa wajasiliamali wadogo badala ya kuendelea kutoa fedha chache ambazo haziwaletei tija kubwa wanufaika wa mikopo ya asilimia 10.


Agizo hilo amelitoa wakati akifungua mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na uongozi wa kata ya Njombe mjini ambapo amesema kuendelea kuwapa mikopo midogo wananchi hakuwapi tija kubwa na mwisho wa siku wengine wanashindwa kurejesha fedha hizo.



Awali Afisa mtendaji wa kata ya Njombe mjini Enoce Lupimo amesema jumla ya vikundi 85 vya ujasiriamali vinanufaika na mafunzo hayo ambayo huku wakiwekeana mikakati mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo.


Baadhi ya wajasirimali hao akiwemo Kipson Tweve wamekiri kuwa mafunzo hayo yatakwenda kuwasaidia katika uendelezaji miradi wanayotekeleza.


Katibu Tawala wilaya ya Njombe Emmanuel George amesema kongamano hilo linapaswa kuwa muarobaini wa malalamiko ya muda mrefu ya wajasiriamali wakidai kuwapo kwa  upendeleo,Hongo na rushwa wakati wa utoaji mikopo hiyo.



Awali akizungumza kwa niaba ya mbunge wa jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika,Mbunge wa Lupembe Edwin Swalle Amesema kutokana na hali za kipato kwa wajasiriamali wengi hapa nchini ndio maana Rais aliagiza yeyote anayeanzisha biashara hatakiwi kulipa kodi mpaka mwaka uishe huku mbunge Mwanyika akiwa na matumaini makubwa na wajasiriamali hao.


Idadi kubwa ya washiriki wa mafunzo hayo ni vijana wajasiriamali ambapo mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM mkoa wa Njombe Bwana Sumuel Mgaya anawataka kuyatumia vizuri mafunzo hayo katika kuliletea heshima taifa kwa kufanya vizuri shughuli zao.



Kata ya Njombe mjini pamoja na mitaa yake imeonesa mfano wa kufanikisha upatikanaji mafunzo kwa zaidi ya wajasiriamali 1000 ambao watakwenda kubadilika kifikra na kuwa na mtazamo wa kujiletea maendeleo kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI