Header Ads Widget

BILIONI 1.165 KUJENGA MRADI WA MAJI NJOMBE DC

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Mradi wa maji wa bilioni 1.165 umesainiwa Katika halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani Njombe na  kampuni ya kitanzania ya Nyagawa Traders  utakaonufaisha wananchi 8,558 kutoka vijiji vitatu vya kata ya Kichiwa kikiwemo kijiji cha Maduma na Igongolo kijiji cha Tagamenda.


Wakazi wa vijiji hivyo  hawajawahi kupata huduma ya maji safi ya bomba  ambapo wamekuwa wakilazimika kufuata maji mabondeni na wengine kuchimba visima vya kuvuta maji kwa mkono hivyo kwa kuona changamoto hiyo serikali ikaona umuhimu wa kumtua ndoo mama kichwani kwa kuanza ujenzi wa mradi huo mkubwa.



Akitoa maelekezo punde baada ya kusaini mkataba huo na mkandarasi,mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa amesema serikali imeguswa na adha kubwa inayowakuta akina mama hivyo anamtaka mkandarasi kuhakikisha anakamilisha ujenzi ndani ya muda wa mkataba huku meneja wa Ruwasa wilaya ya Njombe Mhandisi Elikana Malisa akisema muda wa utatekelezaji ni kipindi cha mwaka mmoja.


Kuanza kutekelezwa kwa mradi huo wa maji kunaibua matumaini mapya kwa wakazi wa vijiji hivyo ambapo baadhi yao akiwemo Ayoub Patson na Beltina Mpango wanasema usalama wa ndoa na maisha kwa baadhi ya akina mama na watoto ulikuwa hatarini kwani walikuwa wakilazimika kufuata maji umbali mrefu mabondeni hivyo kukamilika kwa mradi huo kunakwenda kufungua kurasa mpya kwenye maisha yao.



Wakati Ruwasa  na mkandarasi aliyeingia mkataba wa ujenzi wa mradi huo Said Nyagawa toka kampuni ya Nyagawa Traders  akipewa maagizo ya kutekeleza mradi kwa wakati na kushirikisha wananchi katika kazi lakini mbunge wa Lupembe Mhe.Edwin Swalle na mwenyekiti wa ccm wilaya ya Njombe Mhe. Justin Nusulupila wamesema wanataka kuona mradi huo unatekelezwa kwa mujibu wa mkataba ili kuwatua akina mama ndoo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI