Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea maelezo kuhusu Kituo cha Freedom Park ambacho kimehifadhi kumbukumbu za Wapigania uhuru wa Afrika Kusini, kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndg. Saidi Yakubu jana Machi 16, 2023 jijini Pritoria nchini humo.
Katibu Mkuu Yakubu amemueleza Mhe. Rais Samia kuwa, Tanzania inaendelea kuratibu kupeleka majina mengi zaidi ya Watanzania ambao walisaidia nchi hiyo kupata Uhuru na kupinga ubaguzi wa rangi katika Taifa hilo, ili yahifadhiwe katika vituo vya kumbukumbu vya nchi hiyo, ambapo pia amemueleza kuhusu ushirikiano kati ya vituo vya Ukombozi vya Tanzania na nchi hiyo.
Ziara ya Rais Dkt. Samia katika eneo hilo imehudhuriwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Afrika Kusini Mhe. Zizi Gondwa ( kulia) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Gaudence Millanzi (kushoto).
0 Comments