Header Ads Widget

WAZIRI MAJALIWA: VIONGOZI ITANGAZENI HIFADHI YA BURIGI CHATO

 



NA TITUS MWOMBEKI,Matukio Daima App Kagera 


WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kagera Kasim Majaliwa amewataka viongozi wa mikoa ya Kagera na Geita kuitanga hifadhi ya Burigi chato iweze  kujulikana zaidi na kuongeza watalii.


Ameyasema hayo katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani Biharamulo mkoani kagera ambapo amesema kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suruhu Hassan amedhamilia kukuza uchumi wa nchi  kupitia sekta ya utalii hivyo tumuunge mkono katika hili.


"Rais wetu ameanzisha mpango wakuitangaza nchi na vivutio vilivyopo, akaandaa filamu fupi ya 'Royal Tour' iliyoonyeshwa duniani kote leo hii idadi ya watalii wanaoingia nchini imeongezeka hasa kwenye mikoa mikoa yenye vivutio, jukumu ambalo sasa tunalo  ni viongozi wa mkoa Kagera na Geita kuitangaza hifadhi hii ili watalii wanaotoka Arusha na sehemu mbalimbali  za dunia waje mpaka hapa"



Aidha, amewataka wananchi wa wilaya Biharamulo na Muleba kuchangamkia fursa zitokanazo na ifadhi hiyo kwa kuweka vitega uchumi kama vile hoteli, mighawa pamoja na bishara ndogondogo zitakazowasaidia kuwaingizia kipato pindi watalii watakapokuja kutembelea ifadhi hiyo.


Sambamba na hilo, amewashukuru viongozi wote wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Kagera na  viongozi wa mkoa wa Kagera kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuitangaza ilani ya Chama hicho kwa na kuwataka kutumia vyombo vya habari kuonyesha miradi ambayo imatekelezwa na serikali chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Naye, mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kagera, Nazir Karamagi wakati akitoa neno lake mbele ya mlezi wa chama hicho amesema kuwa chama Cha Mapinduzi mkoani Kagera kiko imara na kimefanya ziara katika wilaya mbalimbali za mkoa huo za kutembelea na kukagua mradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ambapo amesema kuwa miradi iliyotembelewa yote imetekelezwa vizuri na hiko imara.



Sambamba na hilo, Karamagi ameeleza kuwa wakati wakizungukia miradi ya maendeleo ambayo pia walipata fursa ya kukutana na wananchi ili kusikiliza kero zao na kero kubwa waliyokutana nayo ni uwepo wa changamoto ya vitambulisho vya NIDA hasa katika wilaya zilizoko mipakani suala ambalo linapelekea wananchi hao  kukoswa fursa  muhimu.


"Tumezunguka wilaya nyingi katika mkoa wetu na kusikiliza kero zinazowakumba wananchi, changamoto kubwa kubwa ambayo tumekutana nayo katika wilaya nyingi ambazo zipo pembezoni ni changamoto ya vitambulisho vya NIDA suala ambalo pia limepelekea wananchi hao kukoswa fursa muhimu zinazohitaji kitambulisho hicho, kero hii naileta kwako tunaomba utusaidie suala hili uliangalizie namna ya kulitatua"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS