Header Ads Widget

BARABARA YA MCHEPUO TUMAINI - IGUMBILO KUANZA UJENZI -YASSIN


Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa  Daudi Yassin amesema tayari mkataba wa barabara ya mchepuo ya Tumaini - Igumbilo umesha sainiwa hivyo ujenzi wake kuanza mapema .



Yassin amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Lulanzi, Wilayani Kilolo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa.


 Akielezea mafanikio ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020, kuhusu suala la miundo mbinu Yassin alisema kuwa Kuanza Kwa barabara hiyo ni ukombozi mkubwa Kwa mji wa Iringa kuepuka msongamano wa Magari .


Barabara ya mchepuo ya Tumaini -Igumbilo imekuwa ikiuliziwa hasa kutokana na umuhimu wake katika kupunguza msongamano katikati ya mji wa Iringa.


Pia amesema barabara ya Ipogoro - Kilolo imeanza kujengwa.


"Tuendelee kujiunga mkono CCM, tuendelee kumuombea Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Samia Suluhu Hassan, kazi inaendelea kufanyika. Utekelezaji wa Ilani ya CCM unaendelea," amesema Yassin.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS