Na Amon Mtega, Mbinga.
UBORESHWAJI wa Miundombinu mbalimbali ikiwemo ya Elimu unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan umewafanya watoto (Wanafunzi) wengi hasa wa Halmashauri ya Mbinga Mji Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma kupenda kujisomea na kupunguza tabia za utoro.
Akizungumza mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbinga day Eliabu Kikwete wakati akitolea ufafanuzi juu ujenzi wa vyumba vinne vya Madarasa hayo katika shule hiyo ambavyo vimegharimu shilingi milioni 80,ambazo zimetolewa na Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kumepunguza changamoto mbalimbali kwa Wanafunzi hao hasa za utoro na msongamano wa kukaa kwenye Madarasa.
Kikwete amesema kuwa licha ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa hayo lakini umeenda sambamba na uwepo wa viti na meza zake zaidi ya 300 huku awali kabla ya ujenzi huo kufanyika shule hiyo ilikuwa ikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya Madarasa jambo ambalo lilikuwa likisababisha utoro kwa baadhi ya Wanafunzi .
Kwa upande wake kaimu Afisa Mipango katika Halmashauri ya Mbinga mji Eliudi Ngwavi amesema vyumba vya Madarasa hayo vimekamilika na kuwa fedha iliyotumika ni Sh.Milion 80 na kuwa hadi sasa Wanafunzi wanayatumia.
Kaimu Afisa Mipango huyo ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha hizo na kuzielekeza kujenga vyumba vya Madarasa hayo na kuwafanya Wanafunzi waliyowengi kuipenda shule kutokana na Miundombinu yake.
Hata hivyo Ngwavi amepongeza Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga mji Grace Quintene kwa kusimamia ujenzi huo na kuhakisha unakamilika kwa wakati na kuwafanya Wanafunzi wa kidato cha kwanza kutumia madarasa hayo.
Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo Linus Linus amesema kuwa wanajisikia furaha kusoma kwenye Madarasa yenye Miundombinu mbinu yote muhimu ikiwemo na umeme jambo ambalo huwafanya wawe na moyo wa kujituma katika masomo yao.
Mwanafunzi huyo amesema kuwa ubora uliyopo kwenye Madarasa hayo ambayo wanakaa bila msongamano kama siku za nyuma ubora huo umewafanya baadhi ya Wanafunzi wamekuwa wakitamani kama wasitoke katika mazingira ya maeneo ya shule hiyo kutokana kuwa ni sehemu rafiki ya kujisomea.
0 Comments