Header Ads Widget

RC - LINDI “MA DC KASHUGHULIKENI NA WAZAZI WASIOPELEKA WATOTO SHULE”

 


NA HADIJA OMARY _LINDI……



MKUU wa Mkoa wa Lindi bi. Zainab Telack amewataka wakuu wa wilaya wapya mkoani humo  kusimamia maudhurio ya wanafunzi  darasani hasa wanaoripoti kidato cha kwanza  na walioingia darasa la kwanza kwa mwaka wa masomo 2023

 

Telack ametoa maagizo hayo wakati wa hafla fupi  ya kuwaapisha wakuu wa wapya wa wilaya za Liwale, Kilwa na Nachingwea iliyofanyika  jana January 31, 2023 katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa huo Mjini Lindi.

 


Telack  alisema kuwa miongoni mwa mambo ambayo viongozi hao wanatakiwa kuyasimamia katika wilaya zao  ni kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza pamoja na wale wenye umri wa kuanza darasa la kwanza katika Wilaya zao wanakuwa shuleni.

 

“ninawaomba ikawe ndio kazi yenu ya kwanza , kwa sababu tulishaianza naomba mkaendelee nayo kuhakikisha kwamba wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wako darasani lakini wale wenye sifa waliofikia umri wa kuanza darasa la kwanza wote wawepo darasani”

 

Amesema usimamizi huo uende sambamba pamoja na kusimamia maudhurio ya wanafunzi hao waweze kuhudhuria masomo kwa siku 194 ambazo wanafunzi wote wanatakiwa kuwepo darasani kwa mwaka mzima,

 


 

Kwa upande wake Mkuu wa Wialya ya Kilwa Christopha Ngubiagai alisema Swala la uripoti wa wanafunzi wa kidato cha kwanza na wanaotakiwa kuanza darasa la kwanza watatumia taratibu na sheria zote ambazo zipo ili kuhakikisha kila mwanafunzi anakwenda kuripoti shuleni bila kujali ana sare za shule au la.

 

“Hakuna mbadala katika sekta ya elimu, ni vyema wazazi wakatambua kuwa swala la Elimu katika Wilaya ya Kilwa ni swala la kufa na kupona kila mzazi ambae anamtoto ambae anatakiwa kuwa darasa la kwanza au darasa la awali ama kidato cha kwanza tutatumia taratibu sheria, ambazo zipo kwa ajili ya kuhakikisha kila mwanafunzi anakwenda kuripoti shuleni”

 


Nae mkuu wa Wilaya ya Liwale Gooluck Mlinga alisema anafahamu kuwa Wilaya ya Liwale inachangamoto ya wanafunzi kutoripoti katika shule walizochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza sambamba na Watoto wenye sifa ya kuingia darasa la kwanza kutoudhulia masomo

 

Aliesema kwa kushirikiana na watendaji wa Wilaya na Halmashauri atakwenda kusimamia vyema ili kundi hilo la wanafunzi ambao bado wapo majumbani mwao wanaripoti shuleni

 


Nae mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohamed Moyo alisema swala la Watoto kuripoti mashuleni tayari ameshatoa maelekezo wakati wa makabidhiano ya ofisi na mtangulizi  wake kwa maafisa tarafa ili kubaini Watoto ambao walipangwa kuwepo shuleni na hawajaripoti na mahali walipo.

 

“haya ni mapambano na mapambano ni vita na vita si lelemama , haki na ustawi wa mtoto lazima usimamiwe kwa hivyo mtoto akizaliwa ni mali ya serikali   hivyo mzazi yeyote ambae atasababisha mwanae kutokwenda shule kwa kisingizio chochote hatutaweza kumvumilia” alisema moyo

 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS