Header Ads Widget

JELA MIAKA 10 KWA MAUAJI

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma imemuhukumu kifungo cha miaka 10 Antony Japheti (20) mkazi wa kijiji cha Ruchugi wilayani Uvinza mkoani Kigoma kwa kosa la kuua bila kukusudia.

 

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo,Lameck Mlacha Mwendensha Mashitaka wakili wa serikali, Edna Makali aliiambia mahakama kuwa Japheti amefikishwa mahakamani hapo akishitakiwa kwa kosa la kusababisha mauaji ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Jackos Kipara.


Makali aliieleza mahakama kuu kanda ya Kigoma kuwa mshitakiwa alisababisha kifo hicho tarehe 1/9/2021 katika kijiji cha Ruchugi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambapo wawili hao walianza kuzozana  kwa madai ya shilingi 40,000  ambazo mtuhumiwa alikuwa akimdai marehemu.

 

Katika mzozo huo mshitakiwa aliieleza mahakama  kuwa marehemu alikuwa akikaidi kulipa deni hilo  huku akimtishia kumjeruhi kwa kutumia kisu ambapo mzozo ulipozidi ndipo Mshitakiwa alisababisha mauaji hayo.

 

 Akitoa huku ya kesi hiyo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda Kigoma,  Lameck Mlacha alisema kuwa kulikuwa na njia nyingi ambazo mshitakiwa angeweza kuzitumia katika kufikia suluhu ya shauri lake la madai kwa marehemu ikiwa pamoja na kutumia uongozi wa serikali ya kijiji au kufungua kesi ya madai lakini hakufanya hivyo.



Katika hukumu yake Jaji Mlacha alisema kuwa amemuhuku kifungo cha miaka 10 gerezani mshitakiwa huyo ili kuwa fundisho kwa watu wengine wanaochukua hatua mkononi badala ya kufuata mamlaka na taratibu za kiserikali.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI