Header Ads Widget

WANAWAKE MKOANI KILIMANJARO WATAKIWA KUSHIRIKI KATIKA MICHEZO.

 


Wanawake Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kujitokeza katika kushiriki katika michezo mbalimbali ili kumsadia Mh. Rais Samia Suluhu Hasani kuitekeleza ilani ya chama chaapinduzi hususan kwenye michezo.


Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa umoja wa wanawake chama cha mapinduzi ccm wilaya ya Moshi Bi .Teresia Komba wakati alipokuwa katika Tamasha la michezo mbalimbali yalioandaliwa na Uongozi wa Gereza la Karanga Mkoani Kilimanjaro.


"Leo katika bonanza hili la kufunga mwaka 2022 na kupokea mwaka 2023 hapa katika viwanja vya magereza tumeona namna gani watu walivyojitokeza na timu mbalimbali zilivyoweza kushiriki na wameweza kushiriki mashindano yaliyoandaliwa ya mpira wa miguu , pamoja na michezo mengine "Alisema.


Amesema kuwa kupitia michezo vipaji mbalimbali vinaibuliwa pamoja na kuimarisha afya ,na pia inaondoa tofauti kwa kujenga mahusiano mazuri pindi wanapokutana katika michezo .


"Japo changamoto ndogondogo zipo ila naomba tuu wakati mwingine wanawake tuweze kujitokeza kwa kwa wingi na pia waweze kuhamasishwa zaidi katika michezo mbalimbali ili na wao waweze kuibua vipaji ,na sasa hivi pia michezo imekuwa ni sehemu ya ajira " Alisema Komba.


Hata hivyo ametoa rai kwa waandaji wa michezo kuwashirikisha watu wenye uhitaji maalum kwani na wao wana vipaji vya kuonesha kupitia michezo na pia itawasaidia kuwajenga kisaikolojia . 


Aidha wadau mbalimbali walihudhuria katika tamasha hilo la michezo ambapo mmoja wao alikuwa Bw. Samwel Kamandwa Aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Campuni ya Ibra Line foundation amesema kuwa wamejifunza mambo mbalimbali katika bonanza hilo ikiwa ni pamoja na kuona ni jinsi gani watu wanapenda michezo kutokana na kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.


"Kama sisi Ibra line Foundation tunaahaidi kuwaunga mkono popote watakapotuhitaji kwa sababu tunaamini kupitia michezo tutaunganisha jamii na wananchi wote kwa ujumla na makundi mbalimbali , kama mnavyofahamu kwamba kupitia michezo watu wanafanya mazoezi lakini pia vijana badala ya kutumia mda kwenda kutumia madawa ya kulevya lakini kupitia michezo wanaweza wakakaa sehemu moja na kufanya mazoezi na wakaacha zile tabia mbaya ambazo zinaweza kuwaathi "alisema kamandwa. 


Hata hivyo Mkuu wa magereza mkoa wa Kilimanjaro amesema kuwa amesema kuwa tamasha hilo limeweza kuleta timu mbalimbali kutoka mkoa wa Kilimanjaro na mkoa wa Arusha pamoja na nchi jirani ya Kenya .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI