Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA NJOMBE WAWASILISHA KERO ZA KODI KWA WAZIRI DR. KIJAJI

 

Na Gabriel Kilamlya matukio DaimaAPP NJOMBE 

Wafanyabiashara mkoani Njombe wamelalamikia kushindwa kutatuliwa kwa kero mbalimbali za kibiashara zikiwemo sheria kandamizi na mlundikano wa kodi ambazo zimekuwa kikwazo katika sekta hiyo.


Edward Kazimoto,Sebastian Msigwa Anna Mwalongo na Tony Chaula Ni baadhi ya wafanyabiashara waliotoa kero zao kwa Waziri ambao wanalalamikia ukadiliaji Kodi mbaya,sheria kandamizi za biashara pamoja na ubabe wa wakusanya kodi.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amewaonya maofisa wa serikali wenye tabia ya kuwatisha wananchi na kwamba tabia hiyo ikome Mara moja.


Ushuru wa mbao umeonekana kuvuta hisia za wafanyabiashara wengi mkoani Njombe kutokana na Halmashauri kutofautiana katika utozaji Jambo lililomuibua waziri wa viwanda na biashara Dokta Ashatu Kijaji na kutaka kufuatwa kwa shreria za nchi hususani sheria inayotoza ushuru wa mbao kwa asilimia 3 na si vinginevyo.


Madini ya chuma liganga na makaa ya Mawe mchuchuma yaliyopo wilayani Ludewa pia yameendelea kugusa hisia za wananchi wa mkoa wa Njombe ambapo wabunge wa Makambako Deo Sanga na Joseph Kamonga mbunge wa Ludewa wamemuomba Waziri kuwaeleza mchakato ulipofikia.


Festo Sanga Ni mbunge wa Jimbo la Makete ambaye anasema ifike wakati mamlaka zote zinazokusanya kodi na ushuru zikawa pamoja ili mfanyabishara atozwe kodi moja itakayokwenda kugawanywa na mamlaka hizo za Serikali.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI