Header Ads Widget

WAKUU WA WILAYA WAASWA KUFANYA MAAMUZI KWA KUZINGATIA MISINGI YA KISHERIA.

NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.

WAKUU wa wilaya wapya mkoani Kagera wameaswa kufanya maamuzi kwa kuzingatia  misingi ya sheria ili kutatua kero zinawakumba wananchi katika wilaya zao.


Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila katika hafla fupi ya uapisho  wa wakuu wa wilaya ya Bukoba, Muleba na Karagwe ambapo amesema kuwa wakuu wa wilaya wote walioaminiwa na rais ili wakawatumikie wananchi katika kutatua changamoto zinazo wakumba huku akiwasihi kuepuka  kuonevu wakati wakitekeleza majukumu yao.


" Jukumu lenu ni kutafsiri maono ya mweshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassani na kuyaweka katika uharisia hivyo basi katika kutimiza dhima hii nendeni mkatende haki katika kutimiza majukumu yenu na epukeni kuonea watu"


Aidha, mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa wilaya zinazounda mkoa wa Kagera zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa nipamoja na uvuvi haramu, migogoro ya ardhi, wizi wa mifugo na baadhi ya wenyeviti wa vitongoji kusadikika kula rushwa hivyo niwajibu wa wakuu wa wilaya hao kuakikisha wanatatua changamoto hizo.


Sambamba na hilo, Chalamila amesisitiza kuwa wakuu wa wilaya hao wanatakiwa kufanya kazi kwa kushirikiana vyema  na kueshimiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi( CCM)  na kuzingatia mgawanyo wa madaraka.


"Mnamajukumu mengi yakufanya ila majukumu ya muhimu ni pamoja na kujenga umoja na mshikamano katika ngazi zote, kusimamia miradi kwa ufanisi, kuhakikisha mapolisi kata wanashirikiana vyema na viongozi wa ngazi za chini ili kukomesha vitendo viovu ili kudumisha ulinzi kwa raia pamoja na kufanya msako wa nyumba kwa nyumba kubaini watoto ambao wamefahuru lakini hawajaenda shule ili wachukuliwe hatua za kisheria"


Wakuu wa wilaya walioapishwa leo ni pamoja na Erasto Yohana Sima mkuu wa wilaya ya Bukoba, Dkt.Abel Mwendawile Nyamahanga mkuu wa wilaya ya Muleba pamoja na Julius Kalanga Laiser mkuu wa wilaya ya Karagwe.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS