Header Ads Widget

WAKRISTO WA KKKT WAHIMIZWA KUTUNZA MITI ILI KUTUNZA MAZINGIRA..

 

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la la kilitheri Tanzania KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Doct.Askofu Fredrick Shoo ameewaasa wakristo  kuhakikisha kuwa wanajihusisha katika kutunza mazingira yanayowazunguka ikiwa ni pamoja na Kupanda miti katika maeneo yao wanayoishi.


Askofu Shoo ameyasema hayo wakati alipokuwa akiongoza ibada maalum ya kumstaafisha mchungaji Lameck Ndosa  iliyofanyika katika kanisa la KKKT usharika wa Ng'uni uliopo jimbo la hai mkoani Kilimanjaro.


Aidha amewataka viongozi wa kanisa kuhakikisha kuwa wanasimamia mpango uliowekwa na kanisa hilo la kila mwaanafunzi wa darasa la kipaimara kupanda mti pindi anapoanza darasa hilo.


"Niwaombe tu mahali popote mlipo jambo la utunzaji wa uumbaji wa Mungu ni jambo la muhimu sana ,sote tuna wajibu dunia nzima kwani madhara ya mabadiliko ya tabia ya nchi yamekuwa mengi na yanayosababisha kukosekana kwa mvua "

Akizungumza katika ibada mara baada ya kustaafishwa mchungaji Lameck Ndosa amewashukuru viongozi, wachungaji kwa kuonesha ushirikiano katika kipindi chote alchokuwa akihudmu.


"Kipekee niwashukuru washarika kwa kunipa ushirikiano mkubwa wa hali na mali na ushauri katika kufanya kazi ya bwana na kuhakikisha kwamba nastaafishwa kwa heshima" Alisema .


Waumini wa kanisa hillo akiwemo Julius Munuo ameeleza umuhimu wa utunzaji wa mazingira kama wanavyoagizwa na viongozi wa dini na wa Serikali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS