Header Ads Widget

MABINTI WALIOJIFUNGUA UMRI MDOGO NA KUTELEKEZWA WASAIDIWA KUJIAJILI



Pili Simba (aliyesimama) mkazi wa Kijiji cha Ulaya, akiwa katika Saluni yake na kutoa huduma kwa mteja wake aliyefahamika kwa jina la Kulwa  ,ambaye ni mnufaika Kupitia mradi wa kuboresha fursa za vijana wa Kitanzania kuweza kujiajiri ili kuepuka na umasiki(SET)unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la nchini Uswis kupitia Ubalozi wa Uswis nchini Tanzania.


Na Ashton Balaigwa,Morogoro

VIJANA wenye umri kati ya miaka 14 – 24 wakiwemo  Mabinti waliopata watoto wakiwa katika umri mdogo wapatao 490 na kutelekezwa na wenzi wao na kupelekea  kujihusisha na biashara isiyo halali katika  Kata saba za wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro sasa wameokolewa katika biashara hiyo  haramu ya kuuza miili yao baada kupewa mafunzo mbalimbali ya  kufanya biashara na kujikwamua kiuchumi.

 

Mabinti hao wameokolewa

Kupitia mradi wa kuboresha fursa za vijana wa Kitanzania kuweza kujiajiri ili kuepuka na umasiki(SET)unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la nchini Uswis kupitia Ubalozi wa Uswis nchini Tanzania.

 Mradi huo unaotekelezwa  na Shirika la Swisscontact nchini Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini umewapatia mafunzo vijana hao ya  Ujasilimali ikiwemo ushonaji na uanzishaji wa biashara, uchakataji wa vyakula,usindikaji wa maziwa na masuala ya jinsia.

 

Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana hao cha Upendo,kilichopo kata ya Ulaya wilayani Kilosa,Tausi Lyadiga,amesema kabla ya mafunzo hayo baadhi yao walikuwa wakitegemea kujipatia kipato kwa kulaghaliwa na wanaume kufanya ngono.

 

“ Maisha yalikuwa magumu sana unakuta una  mtoto mdogo, anahitaji kula na hela huna ,mwanaume aliyekuzalisha ndio kama hivyo amekutelekeza basi unajikuta unalubunika kwa wanaume wengine kujipatia kipato anaweza kukupata 2000 mpaka 5000”alisema Tausi.

 

Amesema baada ya mafunzo hayo yamewasaidia kuanzisha kikundi  chenye watu 25 na kusindika na kutengeneza maziwa ya mgando,viwazi vilivyosindikwa pamoja na kutoa huduma ya vyakula kama kwenye shughuli mbalimbali na kujipatia kipato.

 

Tausi amesema licha ya kundi hilo lakini baadhi yao kama yeye amejiongeza na kufanya biashara ya mitumba na kujipatia kipato kilichomuwezesha mpaka sasa kusomesha mtoto wake,kusaidia familia na kununua kiwanja ambacho anatarajia kuanza ujenzi wa nyumba yake.

 

“Ni jambo la kuwashukuru sana Shirila la  Swisscotact kupitia mradi wao wa  SET  kwa mafunzo  Hivi sasa hakuna mwanaume anayenibabaisha kwa hela zake,mimi mwenyewe nafanya biashara ya nguo Napata hela,nasomemesha mtoto wangu,nawasaidia wazazi na wadogo zangu lakini kwa sasa ninaanza ujenzi wa nyumba yangu wakati wowote” alisema Tausi.

 

Naye Pili Simba  mkazi wa Kijiji cha Ulaya ,ambaye ni mnufaika wa mafunzo hayo,amesema yamemsaidia sasaivi kuanzisha Saluni ya kike ambaye kwa siku inamuingizia kati ya sh 15,000 mpaka 50,000 kulingana na misimu ya kilimo kitu ambacho kinamuwezesha kumudu maisha na kuondokana na utegemezi kutoka kwa wazazi.

 

“ Mimi nina mtoto ,hivyo biashara ya Saluni ina nipa kipato kikubwa naweza kujimudu kimaisha na pia nafanya shughuli za kilimo cha mpunga na ufuta navyo vinanilipa Napata fedha za kutosha” alisema Pili.

 

Aidha Mnufaika mwingine Zuhena Yasini,alisema baada ya mafunzo hayo yalitolewa na SET kuhusu ujasilimali pamoja na kushiriki katika kikundi chao lakini yeye alimua kujiongeza na kujifundisha Cherehani na baadaye alimua kununua cherehani yake na kuanza kushona nguo huku akifanya biashara nyingine ya kufungua Mgahawa wa kuuza vyakula mbalimbali.

 

“ Elimu tuliopewa na mradi wa SET kwakweli imetufumbua mamcho na kutufanya tuweze kujiamini ,mimi baba watoto hanisaidii chochote  lakini hivi sasa naweza kujimudu kimaisha,nashona nguo Napata hela,nalima lakini nimefungua mgahawa asubuhi nauza supu na hivi navyokwambia tayari nina kiwanja nimeanza kujenga nyumba yangu” alisema Zuhena.


Naye Afisa Mawasiliano na Habari wa Shirika la Swiscontact,Mafunga Isumbi,alisema mradi wa SET umeweza kunufaisha vijana 559 wakiwemo wanaume 69 na wanawake 490 katika kata za Berega,Chanzuru ,Msowero,Mtumbatu,Mvumi,Rudewa na Ulaya kupitia taasisi za MVIWAMORO,CSCA na CRESD ambazo zilipewa kazi ya kutoa mafunzo hayo.

 

Alisema mradi huo umelenga kusaidia vijana wa kiume na wa kike ambao zaidi wa kike waliopata watoto wakiwa bado wadogo ambao wanalea watoto wao bila kuwa na msaidizi baada ya kutelekezwa na wenzi wao na kupitia mradi huo umewawezesha kupata mafunzo ya muda mfupi na kujiajili na kuwawezesha  kujikwamua kimaisha na kuondokana na umasikini.

Amesema  yamemsaidia sasaivi kuanzisha Saluni ya kike ambaye kwa siku inamuingizia kati ya sh 15,000 mpaka 50,000 kulingana na misimu ya kilimo kitu ambacho kinamuwezesha kumudu maisha.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI