Header Ads Widget

Dkt. BATILDA AWAONGOZA WANANCHI WA TABORA KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI YA UPANDAJI MITI.

 Mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani amewaongoza mamia ya wananchi wa manispaa ya Tabora katika uzinduzi ya kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa leo katika kituo cha Afya Maili Tano, kata ya Ipuli.


Katika uzinduzi huo wa wenye kauli ya “Maji ni Uhai na Mti ni Maisha”, Dkt. Batilda alipata nafasi ya kupanda mti ikiwa ni ishara ya uzinduzi huo. Aidha ametembelea wodi ya wazazi ambapo alifanikiwa kuwatembelea Watoto waliozaliwa usiku wa kuamkia leo. Ambapo napo aliwajulia hali Watoto hao na kisha kutoa zawadi ya sabuni, sukari na vitu vingine na kuwapa salamu za mwaka mpya kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan. 


Kwenye hotuba yake, Dkt.Batilda ameweza kufafanua uboreshwaji katika sekta ya afya mkoani Tabora ambapo hospitali 5 za wilaya na shule mpya 12 zilijengwa kwa mwaka 2022. 


Lakini pia amewaomba TFS pamoja na wadau wa mazingira kutoa elimu ya mazingira kwa wananchi ili kuweza kuendeleza zoezi la upandaji miti mkoani Tabora.


Na mwisho alitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuweza kutoa fedha ambazo zimeendelea kuleta miradi mingi ya maendeleo mkoani Tabora.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS