Header Ads Widget

WAFUNGWA WATOROKA NCHINI MEXICO BAADA YA SHAMBULIZI KATIKA GEREZA

 

Makumi ya wafungwa wametoroka katika gereza moja kaskazini mwa Mexico baada ya watu wenye silaha, wanaoshukiwa kuwa wanachama wa genge la dawa za kulevya, kufyatua risasi kwenye gereza hilo.

Wanaume hao walifika nje ya gereza la serikali la Chihuahua wakiwa kwenye magari ya kivita na kuanza kuwafyatulia risasi walinzi, mamlaka inasema.

Watu kumi waliuawa, pamoja na wafungwa wanne, wakati wa shambulio la kikatili katika mji wa mpaka wa Ciudad Juarez. Polisi wanasema wafungwa 24 walitoroka.

Mapigano ndani ya gereza hilo, ambapo wafungwa kutoka makundi tofauti ya wahalifu na wanachama wa magenge ya dawa za kulevya wamewekwa katika vizuizi tofauti, pia yaliwaacha watu 13 na majeraha. Wanne kati yao wanatibiwa hospitalini, wakuu wa magereza walisema. Huko nje jamaa walikusanyika huku na wakisubiri habari za wapendwa wao.

Mwanamke mmoja alisema washambuliaji walikuwa wamevalia nguo nyeusi, walikuwa na silaha bora kuliko polisi, na walikuwa wakifyatua risasi kwa gari lolote lililopita. Jeshi na walinzi wa kitaifa wameitwa kusaidia mamlaka za mitaa kujibu shambulio hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS