Header Ads Widget

DC MPYA LUDEWA NJOMBE AAPISHWA LEO

 Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaApp NJOMBE

Mkuu mpya wa wilaya ya Ludewa Victoria Charles Mwanziva ameapishwa rasmi leo na mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka huku akiomba ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake hayo mapya.


Mheshimiwa Mwanziva ameteuliwa na Rais wa Tanzania siku chache zilizopita akiwa Katibu wa hamasa na chipukizi CCM Taifa ambapo amesema Madini ya chuma Liganga na makaa ya mawe mchuchuma ndio agenda kubwa anayokwenda kushughulikia.


Aidha Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere amesema uongozi ni kama mchezo wa vijiti wa kupokezana hivyo yeye alikuwa wa DC wa 16 na amemwachia Mwanziva.


Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga amemtaka mkuu huyo wa wilaya kwenda kusimamia kikamilifu Utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo amekabidhiwa na mkuu wa mkoa.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS