Header Ads Widget

BOTI YA MWENDOKASI YA RAFIKI 2 YAWA UKOMBOZI KISIWA CHA GOZIBA

 


Wakazi wa Kisiwa cha Goziba kilichopo wilaya ya Muleba mkoani Kagera wameondokana na adha ya usafiri wa majini baada ya wadau wa usafirishaji kampuni ya Songoro Marine Transport kuwapelekea boti ya mwendo kasi itakayowaunganisha wakazi hao na visiwa vingine vilivyomo ndani ya ziwa Victoria.



Wakazi zaidi ya elfu tisa wa kisiwa cha Goziba maarufu kwa shughuli za uvuvi wa dagaa na samaki wakiwa katika mapokezi ya boti ya MV. Rafiki Namba Mbili, Kazi Iendelee, inayomilikiwa na kampuni ya Songoro Marine Transport.


Wananchi hao wa Kisiwa cha Goziba wanasema ukosefu wa usafiri wa uhakika ulisababisha maafa pamoja na kupoteza muda kuwahi katika biashara zao baada ya kusafiri kwa saa kati ya 8 hadi 12 kutoka katika kisiwa hicho kuelekea jiji la Mwanza.



Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro Marine Transport, MAJOR SONGORO amesema mkakati wa kampuni hiyo ni kuwahudumia wananchi kulingana na mahitaji yao ili waweze kuondokana na adha ya usafiri nchini.


Ujio wa boti hii ya kisasa, unatajwa kuchochea maendeleo ya  wananchi wa kisiwa cha Gozba baada ya kuonekana ni mwarobaini miongoni mwa wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi na abiria wanaoingia na kutoka katika kisiwa hicho.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS