Header Ads Widget

UKATILI WA NGONO KWA WANAFUNZI WA VYUO WAPIGWA VITA NJOMBE

 



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakati Tanzania ikiendelea kupinga ukatili wa Kijinsia kupitia siku 16 za kukabilibiana na janga hilo mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema hata  vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wanaume  kwa wanafunzi ikiwemo kuwanunulia simu,gari na hata kuwapangishia nyumba  ni ukatili pia unaopaswa kupigwa vita.


Katika mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani Afrika WILDAF kupitia mradi wa mwanamke Imara ukihusisha wanafunzo wa vyuo vikuu na vyuo vya kati takribani sita nchini Kasongwa amesema ipo haja ya kuongeza nguvu katika kupinga ukatili huo kwa wanafunzi na watoto nchini.


Aidha Kasongwa amesema vyombo vya habari vinatakiwa kuendelea kutangaza habari za ukatili kwa nguvu na hatua zinazochukuliwa ili kukomesha vitendo hivyo.



Susan Kawanga ni Mratibu wa mradi wa Mwanamke Imara toka shirika la Wildaf ambaye amesema wameandaa mdahalo huo katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ukiwa na lengo la kutaka kujadili changamoto zilizopo vyuoni hususani rushwa za ngono na ukatili mwingine katika jamii.


Revocatus Mhinda,Rukia Ngole na Anna Peter  ni baadhi ya wanafunzi toka vyuo vikuu na vya kati  ambao wanakiri kuwapo kwa ukatili vyuoni huku wakisema madawati ya jinsia yaliyoanzishwa yanasaidia Sana kupunguza changamoto ya ukatili huku wakitaka ushirikiano zaidi kwa pande zote.



Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii mkoa wa Njombe Samson Sollo na Afande Andrew Choyo kwa niaba ya mkuu wa Dawati la jinsia toka Jeshi la polisi mkoa wa Njombe wanakiri kuwapo kwa ukatili mkubwa katika mkoa wa Njombe huku kesi za utelekezaji watoto zikiongoza.


Mradi wa mwanamke Imara chini ya shirika la WILDAF unafadhiliwa na Shirika la kimarekani la maendeleo ya kimataifa USAID.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI