Header Ads Widget

TANZANIA KUONDOLEWA VIKWAZO VYA KIBIASHARA 2023

 

Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam

Serikali ya Uingereza imesema kuwa ifikapo mwaka 2023 inatarajia kutekeleza mpango maalumu kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa kuondoa vikwazo mbalimbali vya biashara ikiwemo kodi chechefu ili kuzifanya nchi hizo kuweza kufikia soko lake.


Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Baloziwa Uingereza nchini Tanzania David Concar wakati alipokuwa katika jukwaa la pili la biashara lilowakutanisha wafanyabiashara zaidi ya 100 kutoka Uingereza na Tanzania.


Amesema kuwa, Jukwaa hilo pamoja na mambo mengine ambayo yatajadiliwa katika kukuza biashara baina ya nchi hizo mbili lakini litatoa fursa kwa wafanyabiashara na kuwawezesha kutambua fursa za biashara na uwekezaji zilizopo.


Aidha, amesema kuwa  licha ya Taifa hilo kujiondoa katika umoja wa Ulaya (EU) haitaathiri ushirikiano wao na mataifa ya Afrika kwani watahakikisha wanaondoa kodi ili kuwezesha bidhaa za Tanzania kuingia katika soko shindani.


Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ally Gugu amesema jukwaa hilo litasaidia kuwa na mikakati ya pamoja baina ya Serikali na Taasisi binafsi katika kuongeza thamani katika bidhaa zinazozalishwa Nchini ikiwemo mazao ya Kilimo.


"kutakuwa na jopo linalohusisha wataalam wa biashara na uwekezaji, kusaidia kuboresha mazungumzo kati ya Serikali na sekta binafsi ili kuongeza imani ya wawezaji na biashara" amesema Gugu


Naye, Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza wa Biashara Nchini Tanzania, Lord Walney amesema, Tanzania imepiga hatua kubwa katika kusaidia wawekezaji na wafanyabiashara ambao wametoa mchango wao katika Jukwaa hilo katika kukuza uchumi wa nchi hiyo.


Aidha, amesema zaidi ya wafanyabiashara 20 kutoka Taifa hilo wamehudhuria kongamano hilo lengo ni kuimarisha uwekezaji na kuleta ustawi wa pande zote mbili.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI