Header Ads Widget

MWENYEKITI CCM TANGA ATUMA SALAMU NZITO KWA WAPINZANI ADAI WAMEFIKA MWISHO

 


NA AMINA SAID,MATUKIO DAIMAAPP,TANGA 

Mwenyekiti mpya wa  Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Rajabu  Abdarahman Abdalah amesema kuwa upinzani kwa mkoa wa Tanga umefikia mwisho 


Hayo aliyasema katika mkutano wa hadhara wa Mbunge wa jimbo Pangani na Waziri wa maji Juma Aweso, iliyofanyika wilayani Pangani  kwa ajili ya kusherekea ushindi  wa kushika wadhifa  kuwa Mwenyekiti  kwa kura 1340 kati ya kura 1385.


Aidha mwenyekiti Rajabu alisema kuwa lengo lake kubwa la kugombea nafasi hiyo ni kushika dola ili aweze kusimamia ili kuweza kumsaidia rais Samia suluhu Hassan kuhakiksha nchi inasonga mbele.


Alisema kuwa katika mkoa wa Tanga atahakikisha wapinzani wanasambaratika ili Chama cha Mapinduzi Mkoa iweze kushika dola ili ifikapo  2025 kusiwe na upinzani katika uchaguzi mkuu na mkoa wa Tanga uongoze katika uchaguzi na kumuunga mkono Mh.Samia suluhu Hassan kwa maslahi mapana ya wanatanga.


Kwa upande wake Mnek ambaye Mohamedi Ratico alitoa rai kwa wabunge wote wa mkoa wa Tanga wawe na desturi yankufanya mikutano ya hadhara kwalengo la kujua changamoto za wananchi na kuweza kuzitatua .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS